Barick yatenga billioni tisa kutekeleza miradi 101 ya maendeleo wilayani tarime

GEORGE MARATO TV
0



Na Ada Shadrack,

Nyamongo, Tarime.

KAMPUNI ya dhahabu Barick North Mara, Nyamongo wilayani Tarime imetenga shilingi bilioni 9 katika kipindi cha mwaka 2024 ili kutekeleza Miradi 101 ya maendeleo kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana octoba 11 mwaka huu, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Apolinary Lyambiko alisema hayo na kufafanua kuwa miradi hiyo ni Afya, Elimu, miundombinu ya maji na shughuli nyingine za kijamii.

"Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 tumekamilisha miradi 115 ya maendeleo ya jamii iliyogharimu takriban Bilioni 7.3, pia kwa mwaka huu 2025 tumetenga Bilioni 9 kwa ajili ya kutekeleza wa miradi 101 ya  huduma za kijamii."amesema.

Lyambiko alisema awali kuwa utekelezaji wa huduma hizo ulikwama kutokana na mgongano wa kanuni za (CSR) ambapo tayari kampuni hiyo imeshafanya makubaliano na Halmashauri ya Tarime ambapo miradi imeanza kutekelezwa.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Mgodi huo Francis Uhadi alitoa wito kwa vijana kuacha vitendo vya uvamizi mgodini hapo na kupora mawe badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kupata fedha za miradi ya kilimo, ufugaji.

 Naye Mkuu wa shule ya Msingi Kenyangi  Khadija Sanga alishukuru kampuni hiyo kwa kuwajengea shule iyo ambayo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa alisema majengo mapya ya shule hiyo yamepunguza utoro kwa baadhi ya wanafunzi.

Mkazi wa kitongoji cha Kegonga A Lameck  Chacha ambaye ni katibu wa kilimo biashara ulianzishwa na mgodi huo amesema mradi huo umemuwezeka kusomesha watoto wake watatu na kununua ng'ombe wawili wa maziwa.

Kampuni ya mgodi wa Barick North Mara umekuwa na utaratibu wa kutenga mabilioni kila mwaka kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii (CSR) ili kukuza uchumi wananchi  wa vijijini takriban 11 na Halmashauri ya Tarime 






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top