DCP MUTAFUNGWA AZINDUA ‘KAMPENI YA ONGEA NA KAMANDA’, WANANCHI WAMWAGA YAO YA MOYONI 2\. ‘ONGEA NA KAMANDA’: DCP MUTAFUNGWA AWAPA WANANCHI JUKWAA LA KUELEZA KERO ZAO 3\. DCP MUTAFUNGWA AANZISHA MAZUNGUMZO NA WANANCHI, CHANGAMOTO ZAIBULIWA 4\. WANANCHI WAFUNGUKA, DCP MUTAFUNGWA AZINDUA KAMPENI YA ‘ONGEA NA KAMANDA’ 5\. DCP MUTAFUNGWA KUFUNGUA MILANGO YA MAWASILIANO NA WANANCHI KUPITIA ‘ONGEA NA KAMANDA’ 6\. KERO ZA WANANCHI ZAWEKWA HADHARANI DCP MUTAFUNGWA AKIZINDUA ‘ONGEA NA KAMANDA’ 7\. ‘ONGEA NA KAMANDA’: WANANCHI WAPATA FDCP MUTAFUNGWA AZINDUA ‘ONGEA NA KAMANDA’, WANANCHI WAMWAGA KERO ZAO
Na;Kutoka:Dawati la Habari Polisi Mwanza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amezindua kampeni ya ‘Ongea na Kamanda’ inayolenga kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kukabiliana na changamoto za kiusalama na kudumisha amani na utulivu.
Kupitia kampeni hiyo, wananchi wamepata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na Kamanda wa Polisi, kueleza changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maoni kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa kuboresha usalama.
Akizungumza na wananchi katika stendi ya mabasi ya Nyegezi, Oktoba 10, 2026, DCP Mutafungwa amesisitiza umuhimu wa kusikiliza maoni ya wananchi, wakiwemo madereva, abiria na wafanyabiashara, kuhusu masuala ya usalama yanayowagusa katika shughuli zao za kila siku.
Ameeleza kuwa maoni na changamoto zitakazokuwa zinawasilishwa kupitia mikutano ya hadhara zitapokelewa na kufanyiwa kazi kwa lengo la kuimarisha usalama na kuboresha mazingira ya wananchi katika maeneo yao.
Aidha, kampeni hiyo inalenga kuwapa wananchi nafasi ya kueleza changamoto zinazohusu usalama barabarani, ikiwemo masuala yanayowakabili madereva na abiria pamoja na changamoto zinazoweza kujitokeza katika maeneo ya stendi.
Kwa upande wake, Katibu wa UWT Kata ya Nyegezi, Safia Mohamed, amepongeza huduma nzuri ya Polisi inayotolewa katika kituo cha Polisi Nyegezi.
"Ulinzi katika kata yetu umeimarika vizuri. Afande Mrema alitununulia vifaa vya ulinzi shirikishi, kwa kweli Mungu ambariki sana," amesema Bi Safia.
Naye Salehe Othman pia amepongeza Mkaguzi wa Kata ya Nyegezi, Insp. Abdallah Mrema, kwa kuviwezesha vikundi vya ulinzi shirikishi na kuvipatia vifaa kwa ajili ya kutimiza majukumu ya ulinzi jambo lililofanya kata hiyo kuendelea kuwa na utulivu.






Comments
Post a Comment