Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. NYANSAHO: KITUO CHA FORODHA MANYOVU KUONGEZA MAPATO NA KUIMARISHA USALAMA

 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu, kilichopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, ni hatua muhimu katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kurahisisha huduma za forodha pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za mpakani. Dkt. Nyansaho ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Kigoma, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya kimkakati, ikiwemo Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu na ujenzi wa Barabara ya Kabingo–Kasulu Manyovu. Amesema kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa na manufaa makubwa kwa Serikali na wananchi kwa kuwa kitaweka pamoja huduma mbalimbali zinazohusiana na shughuli za forodha, hivyo kupunguza usumbufu na kurahisisha utoaji wa huduma kwa watu wanaotumia mpaka huo. Waziri Nyansaho, amesema uwepo wa kituo hicho unatarajiwa pia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa shughuli zinazofanyika mpakani, sambamba na kuhakikisha Serikali inapata mapato yanay...

MAGANYA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MEATU, ATOA MSUKUMO KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ndugu Fadhili Rajabu Maganya, ameendelea na ziara yake Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyokusudiwa. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Maganya ameambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndugu Shamsa Mohamed, pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali. Akiwa Shule ya Msingi Meatu, Mwenyekiti Maganya amekagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa wenye thamani ya Shilingi milioni 125, unaolenga kuongeza nafasi za kujifunzia na kuweka mazingira bora kwa wanafunzi na walimu. Aidha, ametembelea Shule ya Sekondari Meatu, ambako amekagua miundombinu ya shule hiyo na kupata taarifa kuhusu maendeleo pamoja na hali ya mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Maganya pia ametembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Wazazi Wilaya ya Meatu pamoja na ...

BALOZI KHAMIS OMAR AALIKWA MAZUNGUMZO YA UFADHILI ENDELEVU WA AFYA AFRIKA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili Addis Ababa, Ethiopia, kushiriki kama mwanajopo katika Mazungumzo ya Mawaziri wa Fedha kuhusu ufadhili endelevu wa afya barani Afrika katika kipindi cha ufinyu wa bajeti na juhudi za nchi kujitegemea katika masuala ya afya. Mhe. Omar amepokea taarifa kuhusu maandalizi ya ushiriki wake na agenda za mkutano huo kutoka kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia. Mazungumzo hayo yanawakutanisha Mawaziri wa Afya na Fedha, washirika wa maendeleo na viongozi wa kikanda kujadili changamoto za kifedha zinazoathiri upatikanaji wa huduma za afya kwa wote (UHC), ikiwemo kupungua kwa misaada kutoka nje, ufinyu wa bajeti na kuongezeka kwa mzigo wa madeni. Mkutano huo unafanyika kabla ya Kikao cha 76 cha Kamati ya Kanda ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Afrika.

RAIS MUSEVENI AWAASA MAAFISA WASTAAFU KUTUMIA BUSARA MAFAO YAO

 Rais wa Uganda na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), Yoweri Kaguta Museveni, amewaaga rasmi maafisa wakuu 19 wa jeshi hilo waliostaafu, akiwataka kutumia kwa busara mafao na akiba zao ili kujenga maisha salama na yenye uhakika wa kifedha baada ya utumishi. Akizungumza katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Entebbe, Rais Museveni amewapongeza maafisa hao kwa miaka yao ya utumishi na mchango wao katika kujenga na kuimarisha UPDF pamoja na kulinda amani na usalama wa Uganda. Amewataka wastaafu hao kuepuka kufanya maamuzi ya haraka katika matumizi ya mafao yao, badala yake kuelekeza fedha katika uwekezaji salama na wenye uwezo wa kuzalisha kipato cha kudumu. Museveni ametaja uwekezaji katika hati fungani za Serikali kuwa miongoni mwa maeneo salama, akieleza kuwa unaweza kumwezesha mstaafu kupata mapato ya riba bila kulazimika kushiriki moja kwa moja katika uendeshaji wa biashara. “Ukiweka Shilingi milioni 600 na ukapata asilimia 15, mwishoni mwa mwaka hiyo n...

WANAFUNZI 95 WAENDA INDIA KUSOMEA AI, UHANDISI

 Na Mwandishi Wetu Zaidi ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link katika mwaka 2026. Wanafunzi hao walioondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa. “Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tun...

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili, Agosti 23, 2026, katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi. Alipowasili hospitalini hapo, Dkt. Mwigulu ametembelea wodi mbalimbali, zikiwemo Wodi ya Mama na Mtoto na Wodi ya Upasuaji, ambako amezungumza na wagonjwa pamoja na ndugu zao na kusikiliza maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo na changamoto wanazokabiliana nazo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na mazingira ya utoaji wa huduma hospitalini hapo. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule; pamoja na viongozi wa Hospitali hiyo.