Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, ameendelea kusisitiza utatuzi wa kero za wananchi kwa vitendo baada ya kufanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, ambapo alisikiliza changamoto mbalimbali na kutoa maelekezo ya utekelezaji wa haraka. Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Julai 9, 2026, Mhe. Mtambi aliliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kuanza taratibu za kuanzisha kituo kidogo cha polisi katika eneo la Suguti, kufuatia ombi la wananchi waliobainisha kuwa uwepo wa kituo hicho utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa wakazi pamoja na mali zao. "Wananchi wanahitaji huduma za usalama karibu yao. Jeshi la Polisi lifanye taratibu za kuanzisha kituo kidogo cha polisi katika eneo hili ili kuongeza ufanisi wa ulinzi na usalama," amesema Mhe. Mtambi. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliunda kamati maalumu ya kuchunguza malalamiko ya uchafuzi wa mazingira katika Kitongoji cha Karusenyi,...
Marato tv - Sauti ya Jamii