Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeridhia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa mamlaka na muswada wake unatarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Reuben Kwagilwa, wakati wa kikao kazi baina ya NEMC na wadau wenye viwanda. Naibu Waziri alisema serikali kwa upande wake imeshakamilisha mchakato mzima wa kuifanya iwe mamlaka kamili kwa kufanya mashauriano na wadau mbalimbali na wataalamu washauri. Alisema mchakato huo utawasilishwa bungeni na baada ya hapo wananchi watapewa nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu muundo wa mamlaka hiyo na kutaka wananchi kujitokeza kutoa maoni wakati huo “Niwatoe hofu wananchi na wadau kwamba kwa NEMC kuwa mamlaka haimaanishi kwamba itakuwa inafanyakazi kwa mabavu mabavu au kwamba itamwonea mtu, badala yake ndipo itafanyakazi zake kistaarabu zaidi kwa hiyo msiogope,” alisema Aidha, aliitaka NEMC kuhakikisha wananchi watakapoitwa...
Marato tv - Sauti ya Jamii