Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 15 Mei 2026 amewasili mkoani Mara kwa shughuli za Kikazi. Pamoja na mambo mengine Mhe. Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki Mazishi ya Bw. Boniface Makene, aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, yatakayofanyika katika Kijiji cha Mabui, Musoma Vijijini mkoani Mara, kesho tarehe 16 Mei 2026.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.





Comments
Post a Comment