Skip to main content

Afrika Yahimizwa Kujenga Mustakabali Salama kwa Watoto


Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Neema Mwigulu Nchemba, ametoa wito  kwa viongozi na wadau wa Afrika kuweka kipaumbele katika ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili wa kidijitali. 

Akizungumza jijini Nairobi, Kenya  Mei 12, 2026, katika  Mkutano wa Wenza wa Mawaziri wakuu wa nchi za Afrika, uliofanyika Pembezoni  mwa Mkutano wa “Africa-Forward Summit” ukilenga kujenga mazingira salama ya kidijitali kwa watoto wa Afrika katika ulimwengu unaoendeshwa na Akili Unde (AI). Bi.Nchemba alisisitiza kuwa mustakabali wa bara la Afrika hautategemea tu vigezo vya kiuchumi, bali uwezo wa watoto kujifunza na kuvumbua katika nafasi ya kidijitali bila hofu ya unyanyasaji.




Katika hotuba yake, alibainisha kuwa ingawa teknolojia ya Akili Bandia (AI) inatoa fursa kubwa katika sekta za elimu, afya, na ujasiriamali, imeleta pia hatari mpya na halisi. Alitaja changamoto kama vile uonevu mtandaoni, unyanyasaji wa kijinsia unaochochewa na AI, na ulaghai kama vitisho vinavyovuruga utu na maendeleo ya watoto barani Afrika.

Ameeleza hatua zilizopigwa na Tanzania, ikiwemo kufanya marekebisho ya Sheria ya Mtoto (Sura ya 13) na kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Aidha, alikumbusha  Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi wa Watoto Mtandaoni iliyoanzishwa Februari 2024 na kuundwa kamati maalum ya wadau mbalimbali ili kuhakikisha mazingira salama kwa watoto.

Mkutano huo, uliandaliwa na Kuongozwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mama Rachel Ruto ambapo ulihitimishwa kwa wito wa dharura wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na sheria madhubuti. 






Comments

George marato tv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.