Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Amb. Hoyce Temu Affirms Tanzania’s Commitment as IPU Elects First Woman Secretary-General

By Prosper Makene  The new Inter-Parliamentary Union Secretary-General was elected today, with Ambassador Anda Filip winning 229 out of 321 votes. She will assume office in July 2026, becoming the first woman to lead the IPU in the organization’s 140-year history.  Tanzania cast its vote for Ambassador Anda Filip, who previously visited Tanzania and advised the Central Committee to approve Arusha as the venue for the 153rd IPU Assembly in October. Ambassador Hoyce Temu, Deputy Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Office in Geneva and manager of the IPU desk from the IPU’s headquarters in Geneva, said from Turkey that Tanzania backs Ambassador Anda Filip, noting her visit to the country and her role in recommending Arusha as the host city for the upcoming Assembly. She described the election as a milestone for both gender representation and parliamentary cooperation. Temu also confirmed that the Tanzanian delegation at the IPU is led by the Right Honorable...

Waziri Ulega Amwaga Sifa Kwa Nyansaho Kwa Kufanikisha Billion 1.4 Kuchangwa ndani ya Saa Moja

 KIASI cha zaidi ya bilioni 1.4 kimekusanywa katika harambee kubwa ya kuchangia ujenzi wa shule na zahanati katika kijiji cha Musati, wilayani Serengeti mkoani Mara, hafla iliyoongozwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega. Harambee hiyo iliyofanyika Jumamosi (Aprili 18, 2026) imeandaliwa na Taasisi ya Nyansaho (Nyansaho Foundation) chini ya Mwanzilishi na Mwenyekiti wake, Dkt. Rhimo Nyansaho (MB) ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Akizungumza katika hafla ya harambee hiyo, ambayo ilitanguliwa na uzinduzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato ,Musati Central pamoja na nyumba ya mchungaji, Mwenyekiti wa Nyansaho Foundation, Dkt. Rhimo Nyansaho ambaye pia ni waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, amesema taasisi yake imejikita kusaidia miradi ya kijamii hususan elimu na afya. Amesema miradi hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Nyansaho kwa thamani ya TZS 500 milioni. Sambamba na hayo amewashukuru viongozi Mbalimbali na Wananchi kwa michango hiyo, amba...

Tume ya Madini Morogoro ,Fadev, na Undp .Wawapiga Msasa Wachimbaji Wadogo

Tume ya Madini kwa ushirikiano wa  Shirika la Maendeleo ya Umoja wa  Mataifa (UNDP) pamoja na Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji Mdogo (FADev) wameendelea kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Morogoro ikiwa ni Mkakati wa serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo Mradi unaofadhiriwa na UNDP.  Akiongea na Wachimbaji wa madini ujenzi katika Mkoa wa Morogoro Afisa Program kutoka FADev  Bi Rehema Mkuli amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wachimbaji wadogo wanaojihusisha na madini ya ujenzi na viwanda, hususani madini ya kokoto kwa lengo la kuboresha uelewa wao wa kitaalamu na kuhamasisha mbinu salama na zenye tija katika shughuli za uchimbaji. Pia Bi Rehema amesema wachimbaji hao wanajifunza juu ya mbinu za Msingi za Uchoraji wa Ramani za Kijiolojia (Basic Geological Mapping), Usanifu salama na bora wa mashimo (Safe and Efficient Pit Design) Aidha Kwa upande wa wakufunzi kutoka ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro  Mjiolojia Asifiwe  Waksoni Ng...

Sitovumilia Mwalimu Kuonewa Au Kutotendewa Haki - Prof. Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI, Bahi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema iwapo atapewa taarifa ya uhakika ya afisa yeyote anayepaswa kuwahudumia walimu na kutatua kero zao, kwamba amemuonea au kutomtendea haki mwalimu yeyote hatosita kumuondoa katika cheo alichonacho. Prof. Shemdoe ametoa tahadhari hiyo Aprili 17, 2026 akiwa wilayani Bahi, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, saba, kidato cha pili na cha nne wa wilaya ya Bahi, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani humo. “Tutatue kero za walimu kwa wakati, nitakuwa mkali na sitomfumbia macho afisa yeyote wa idara ya elimu atakayemuonea au kutomtendea haki mwalimu, nitachua hatua ya kumuondolea cheo alichonacho  kwani atakuwa ameugusa moyo wangu,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe ameanisha kuwa, kuna maeneo yana changamoto ya kuwahudumia walimu akitoa mfa...

Silent Ocean Yaahidi Kuendelea Kudhamini Bunge Marathon Kwa Miaka Mitano Zaidi

KAMPUNI  ya kimataifa ya usafirishaji wa mizigo ya Silent Ocean, maarufu kama “Simba wa Bahari”, imetangaza kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa Bunge Marathon kwa kipindi cha miaka mitano zaidi, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kulinda afya zao. Akizungumza leo Aprili 18, 2026 katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma wakati wa mbio hizo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ndg. Mohammed Soloka, amesema Kampuni hiyo imejipanga kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na Serikali pamoja na jamii katika nyanja mbalimbali za maendeleo. “Tutaendelea kuwa sehemu ya Serikali yetu kwa kushirikiana katika kuimarisha huduma kwa jamii na kuhakikisha wananchi wanapata elimu na huduma bora kupitia kampuni ya Silent Ocean,” amesema Soloka. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake mkubwa uliowezesha mafanikio ya Bunge Marathon msimu wa tatu, akieleza ku...