Tume ya Madini Morogoro ,Fadev, na Undp .Wawapiga Msasa Wachimbaji Wadogo

GEORGE MARATO TV
0


Tume ya Madini kwa ushirikiano wa  Shirika la Maendeleo ya Umoja wa  Mataifa (UNDP) pamoja na Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji Mdogo (FADev) wameendelea kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Morogoro ikiwa ni Mkakati wa serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo Mradi unaofadhiriwa na UNDP. 

Akiongea na Wachimbaji wa madini ujenzi katika Mkoa wa Morogoro Afisa Program kutoka FADev  Bi Rehema Mkuli amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wachimbaji wadogo wanaojihusisha na madini ya ujenzi na viwanda, hususani madini ya kokoto kwa lengo la kuboresha uelewa wao wa kitaalamu na kuhamasisha mbinu salama na zenye tija katika shughuli za uchimbaji.

Pia Bi Rehema amesema wachimbaji hao wanajifunza juu ya mbinu za Msingi za Uchoraji wa Ramani za Kijiolojia (Basic Geological Mapping), Usanifu salama na bora wa mashimo (Safe and Efficient Pit Design)

Aidha Kwa upande wa wakufunzi kutoka ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro  Mjiolojia Asifiwe  Waksoni Ngala amewalezea wachimbaji juu ya Uchoraji wa ramani za kijiolojia, na kuwataka wachimbaji  kujifunza zaidi  juu ya  utambuzi wa aina mbalimbali za miamba na kuelewa madini yanayopatikana ndani yake. 



Ujuzi huu unasaidia kuongeza ufanisi katika utambuzi wa rasilimali, kupunguza uchimbaji wa kubahatisha, na kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji.

Mafunzo haya yamelengwa kufanyika katika mikoa minne kati ya mikoa nane iliyofanyiwa utafiti wa Madini ya Maendeleo (Development Minerals). Mikoa hiyo ni Singida, Dodoma, Morogoro na Tanga.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top