Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Apokea Taarifa na Kuipongeza PPRA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bw. Dennis Simba, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026. Rais Samia amempongeza mkurugenzi mkuu wa PPRA kwa kazi nzuri ya usimamizi wa manunuzi ya umma huku akimtaka kuzitaja taasisi zinazoshindwa kufuata taratibu za manunuzi katika taarifa yake itakayowasilishwa mwaka ujao wa fedha.

Wafanyabiashara Waomba Msako Mkali wa Bidhaa Bandia Zinazoletwa Nchini Kunusuru Afya za Walaji

Na mwandishi wetu Jovina Massano. Musoma. WAFANYABIASHARA mkoani Mara waiomba Serikali kupitia Tume ya ushindani( FCC) kufanya msako mkali  kwa wauzaji na wasambazaji wa bidhaa bandia ili kunusuru afya za walaji. Wamemweleza Meneja Kanda ya Ziwa wa Tume ya Ushindani (FCC) Frank Mdimi kuwa baadhi ya wafanyabiashara  wamekuwa wakienda kwenye viwanda vya nje ya nchi na kuomba kutengenezewa bidhaa zisizo na ubora zinazohatarisha afya ya mlaji. Wafanyabiashara baadhi wanaokwenda kuchukua bidhaa nje ya nchi hawajali afya za walaji wanaangalia faida pekee kwa kuleta bidhaa za ghalama nafuu pasipo kuangalia athari zake. Hivyo wameiomba Serikali kupitia Tume ya Ushindani FCC kufanya msako wa mara kwa mara ili kuweza kuondoa kabisa bidhaa bandia na kuweza kuwa na bidhaa zenye ubora zenye kulinda afya za walaji. Juma Chacha amesema"madhara yatokanayo na bidhaa bandia hayabagui ukoo unaweza ukaleta unasema nawauzia wengine kumbe na ndugu zako wanaotumia wanakuwa wahanga wa bidhaa bandia n...

Serikali Yaongeza Nguvu Ujenzi Wa Barabara Kukabiliana Na Msongamano Na Kukuza Biashara

Na,Saleh Lujuo-Dodoma: SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imejipanga kuongeza uwekezaji mkubwa katika ujenzi na upanuzi wa barabara nchini ili kuendana na kasi ya ukuaji wa miji, ongezeko la magari na mahitaji makubwa ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi. Hatua hiyo inalenga kuboresha mtiririko wa usafiri, kupunguza msongamano wa magari na kufungua zaidi fursa za biashara katika ngazi ya ndani na kikanda. Akizungumza leo jijini Dodoma, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Ephatar Mlavi, amesema serikali imeongeza rasilimali katika sekta ya miundombinu ili kuhakikisha barabara za kitaifa zinajengwa, zinaboreshwa na zinatunzwa kwa viwango vinavyoendana na ukuaji wa uchumi. Amesema ongezeko la idadi ya magari pamoja na kuimarika kwa usafirishaji wa mizigo kutoka nchi jirani ikiwemo DRC, Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi na Zambia, limeongeza mahitaji ya miundombinu ya barabara, hali inayolazimu serikali kuchukua hatua madhubuti za kuongeza uwezo wa baraba...

Rais Dkt. Mwinyi Akutana na Mewata, Aunga Mkono Mkutano Mkuu Wa Madaktari Wanawake Afrika Kufanyika Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na uongozi wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) uliofika Ikulu, Zanzibar leo tarehe 30 Machi 2026. Ujumbe huo ulioongozwa na Rais wa chama hicho, Dkt. Mary Mwanyika Sando, umewasilisha dhamira ya kuandaa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Vyama vya Madaktari Wanawake Afrika, unaotarajiwa kufanyika Zanzibar tarehe 05 Mei 2027. Mkutano huo unatarajiwa kuwashirikisha madaktari takriban 400 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika. Akizungumza katika kikao hicho, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa kufanyika kwa mikutano ya kimataifa nchini ni tija kubwa na fursa muhimu ya kuitangaza Zanzibar kimataifa pamoja na kuimarisha sekta ya utalii. Ameeleza kuwa washiriki wa mikutano hiyo huwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar wanaporejea katika nchi zao. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza juhudi za MEWATA kwa kuamua kuandaa mkutano huo Zanzibar, akisisitiza kuwa ni fursa muhimu kwa maendeleo ya sekta ya...

Makaa ya Mawe Kuchochea Maendeleo ya Viwanda Nchini Tanzania

▪️ Waziri Mavunde asikiliza na kutatua changamoto za wadau ▪️ Wadau wa makaa ya mawe waipongeza Serikali kwa kuwasikiliza ▪️ Waahidi kuongeza uzalishaji ili kukuza mapato ya Taifa ▪️ Kiwanda cha chuma kujengwa Dodoma na kutumia tani 20,000 za makaa ya mawe kwa mwaka 📍Dodoma Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema makaa ya mawe yana nafasi ya kimkakati katika kuharakisha mageuzi ya uchumi wa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda, akibainisha kuwa rasilimali hiyo si tu chanzo cha nishati bali pia ni mhimili wa kuongeza thamani ya madini na malighafi nyingine za viwandani. Amesema kupitia matumizi sahihi ya makaa ya mawe, nchi inaweza kupunguza utegemezi wa bidhaa za nje, kuongeza uzalishaji wa ndani na kuimarisha mnyororo wa thamani katika sekta mbalimbali ikiwemo  nishati, viwanda na madini. Akizungumza leo Machi 30, 2026 katika kikao na wadau wa makaa ya mawe kilichofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Madini, Jijini Dodoma, Mhe. Mavunde amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kusikiliz...

Mhandisi Samamba Asisitiza Kuimarishwa Usimamizi wa Usalama Sekta ya Madini

📍Mwanza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka watendaji wa Tume ya Madini hususan Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuimarisha usimamizi wa mazingira katika shughuli za uchimbaji madini kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara, hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua, ili kuzuia ajali zinazoweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifo. Mhandisi Samamba ametoa wito huo wakati akifungua Kikao cha Pili cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Tume ya Madini kilichofanyika jijini Mwanza, kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, viongozi kutoka Wizara ya Madini, Ofisi ya Kamishna wa Kazi,Mhandisi Samamba Asisitiza Kuimarishwa Usimamizi Wa Usalama Sekta Ya Madini TUGHE pamoja na wakurugenzi, mameneja na wawakilishi wa Ofisi za Maafisa Madini Wakazi kutoka mikoa mbalimbali nchini. Amesisitiza kuwa usalama wa wachimbaji unapaswa kuwa kipaumbele cha ...