Wafanyabiashara Waomba Msako Mkali wa Bidhaa Bandia Zinazoletwa Nchini Kunusuru Afya za Walaji

GEORGE MARATO TV
0


Na mwandishi wetu Jovina Massano. Musoma.

WAFANYABIASHARA mkoani Mara waiomba Serikali kupitia Tume ya ushindani( FCC) kufanya msako mkali  kwa wauzaji na wasambazaji wa bidhaa bandia ili kunusuru afya za walaji.

Wamemweleza Meneja Kanda ya Ziwa wa Tume ya Ushindani (FCC) Frank Mdimi kuwa baadhi ya wafanyabiashara  wamekuwa wakienda kwenye viwanda vya nje ya nchi na kuomba kutengenezewa bidhaa zisizo na ubora zinazohatarisha afya ya mlaji.






Wafanyabiashara baadhi wanaokwenda kuchukua bidhaa nje ya nchi hawajali afya za walaji wanaangalia faida pekee kwa kuleta bidhaa za ghalama nafuu pasipo kuangalia athari zake.

Hivyo wameiomba Serikali kupitia Tume ya Ushindani FCC kufanya msako wa mara kwa mara ili kuweza kuondoa kabisa bidhaa bandia na kuweza kuwa na bidhaa zenye ubora zenye kulinda afya za walaji.

Juma Chacha amesema"madhara yatokanayo na bidhaa bandia hayabagui ukoo unaweza ukaleta unasema nawauzia wengine kumbe na ndugu zako wanaotumia wanakuwa wahanga wa bidhaa bandia na wapatapo maradhi yatokanayo na bidhaa hizo nawe unaghalamika na kuiletea familia yako hasara ni vema tukafuata utaratibu sahihi hata kama ni soko huria".

Meneja Kanda ya Ziwa wa Tume ya Ushindani FCC Frank Mdimi amesema elimu inaendelea kutolewa  kwa wote lengo kuwajengea uwezo walaji kutambua bidhaa bandia na kufanya maamuzi ya kutotumia bidhaa hizo.

Aidha amewaeleza wafanyabiashara kuwa   chini ya Kifungu cha 9 Cha Sheria ya Alama za Bidhaa (CAP.85 R.E 2023 swali namba 1-4 kukutwa unauza, kuzalisha kuingiza na kusambaza ni kosa kisheria. 

Ameendelea kufafanua kuwa Kifungu cha 9(1) (a) (i) Kimeeleza kufanya kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka isiyozidi 5 ama faini ya kiasi cha TZS 10M.

Kifungu hicho hicho cha 9(1)(a) (ii) kimeendelea kuweka bayana faini hiyo inaweza tozwa kwa kuangalia thamani ya mzigo uliokamatwa ikiwa ni mara tatu ya thamani ya mzigo huo.

Pia Kifungu hicho  kipengele (b) kama mkosaji amefanya kosa katika hali ya mrudio mtuhumiwa atapewa adhabu ya kifungo kisichozidi miaka 15 na faini yake ni kiasi kisichozidi 50M ama thamani ya mzigo wake mara tano.

Hivyo ametoa rai kwa wafanyabiashara kutojihusisha na uuzaji na usambazaji bidhaa bandia kuepuka adhabu hizo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top