Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bw. Dennis Simba, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026.
Rais Samia amempongeza mkurugenzi mkuu wa PPRA kwa kazi nzuri ya usimamizi wa manunuzi ya umma huku akimtaka kuzitaja taasisi zinazoshindwa kufuata taratibu za manunuzi katika taarifa yake itakayowasilishwa mwaka ujao wa fedha.



