Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Katambi Akutana na Msajili wa Silaha Nchini

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amekutana kwa Kikao Kazi na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Usajili wa Silaha,Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi,ACP Berthaneema Mlay ambapo wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo Sera za Umiliki wa Silaha. Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Silaha,Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi,ACP Sebastian Madembwe. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi ndogo ya waziri,jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Awasili Nchini Guinea ya Ikweta, Kumwakilisha Rais Samia

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 26 Machi 2026 amewasili Jijini Malabo nchini Guinea ya Ikweta, ambapo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, utakaofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Machi 2026. Katika Mkutano huo, Tanzania itapata fursa ya kuwasilisha vipaumbele vyake vya Kitaifa pamoja na kuchangia kuunda mwelekeo wa mikakati mipya ya jumuiya hiyo, inayoelekea kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano huo ni mwendelezo wa jitihada za kuendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kikanda na kimataifa, na kudhihirisha mchango wa nchi katika mijadala ya maendeleo na ushirikiano wa kimataifa. Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano huo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano w...

Mwili wa William Lukuvi Wapelekwa Nyumbani Kwake Dodoma

 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Marehemu Mhe. William v. Lukuvi ukitolewa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa kuelekea nyumbani kwake , leo tarehe 26 Machi 2026, Area D jijini Dodoma. Mhe. Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa Matibabu.

Pbpa Yaagizwa Kuharakisha Upokeaji na Usazambazaji wa Mafuta Nchini

Dar es Salaam Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius John Ndejembi ameutaka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kuhakikisha kuwa maghala yote makubwa ya usambazaji wa mafuta yanapata bidhaa hiyo kwa wakati, ili kuimarisha upatikanaji wake nchini. Hayo yamesemwa  leo Machi 26, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na viongozi wa PBPA, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kampuni ya TIPER kwa lengo la kujadili hali ya upokeaji wa mafuta yanayoingia nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi ameielekeza PBPA kuweka mfumo madhubuti wa upangaji wa ratiba ya ushushaji wa mafuta (sequencing) ili kuhakikisha maghala yote makubwa yanayohusika na usambazaji yanapata mafuta kwa usawa na kwa wakati.  Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa mafuta katika maeneo mbalimbali ya nchi. Aidha, ameeleza kuwa Serikali imekubaliana kuharakisha ushushaji wa meli za mafuta zinazoingia nchini, hususan kwa ajili ya matumizi ya ...

Rais Samia Ashiriki Kikao cha Baraza la Uongozi Umoja wa Afrika

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), akishiriki Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Afrika (African Union Bureau of Assembly) kilichofanyika kwa njia ya mtandao, tarehe 26 Machi, 2026, Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.  Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye.

Dkt. Mwigulu: Tuendelee Kumuombea Mhe. Lukuvi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki jana Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma. Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu amesema: “Kwa niaba ya Serikali natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa. Jambo hili zito, gumu kulielewa, gumu kulipokea.” …Lakini ndio limeshatufika na sote hatukutarajia maana Mheshimiwa Waziri alikuwa kazini. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuifariji familia. Mwenyezi Mungu awaimarishe kwa sababu yeyé ndio mfariji mkuu,” amesisitiza. Vilevile, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kuihakikishia familia kwamba Serikali itaendelea kuwa pamoja nayo katika kipindi hiki chote cha majonzi. Viongozi wengine waliokuwepo msibani hapo ni pamoja na Naibu Spika, Daniel Siro, Waziri wa Nc...