Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kishindo Cha Dkt. Migiro, Akiwasili Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 13.1.2026 amewasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuzungumza na mabalozi wa mashina wa wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam. Leo ikiwa ni hitimisho ya ziara yake ya kimkakati ya siku tatu mkoani Dar es salaam iliyobeba kauli mbiu isemayo #ShinaLakoLinakuita#. Tayari ameshafanya ziara katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Kinondoni na Ubungo.

Rais Samia Avunja Rekodi Kuwa Rais wa Pili Tanzania Kufungua Mkutano wa Chama Cha Mahakimu na Majaji (Tmja) Tanzania, Asisitiza Haki Mahakamani

Leo tarehe 13/1/2026 Rais wa jamuhuri ya Muungano wa tanzania amevunja rekodi kwa kuwa *Rais wa pili nchini tanzania* kufungua mkutano wa majaji na mahakama tangu mwaka 1984 ambapo *Hayati Mwl. Julius K nyerere* alihutubia mkutano huo. Katika mkutano huo Rais samia ameiomba mahakama kuwa chombo huru na chenye utoaji wa haki kama ilivyoainishwa kwenye *ibara ya 107 na 107B* ya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia rais ameahidi kuwa serikali itaendelea kuuheshimu na kuulinda uhuru wa mahakama kama sheria za nchi zinavyotaka. Rais samia amepasua mwamba kwa kuwaomba majaji na mahakimu kutendea haki watu, amesema *sio sahihi watu kuwekwa mahabusu au kufungwa kwa makosa ya kubambikiwa,* amewaomba majaji kuwa huru na kufanya kazi kwa kujipima ili kuondoa uonevu kwa watu wasio na hatia. Rais samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya mahakama, mfano jengo la mahakama la pili kwa ukubwa zaidi barani afrika na la sita kwa ukubwa duniani la *Judiciary square* n...

Shule Zote 18055 za Msingi Zipo Tayari Kupokea Wanafunzi- Prof. Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameridhishwa na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza katika Shule ya Msingi Iyumbu jijini Dodoma, na kuuarifu umma kuwa maandalizi katika shule zote za msingi 18055 yamekamilika na zipo tayari kupokea wanafunzi kuanzia Januari 13, 2026. Prof. Shemdoe amesema, ameitembelea shule hiyo ya Msingi Iyumbu leo Januari 12, 2026, ili kujiridhisha na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza darasa la awali na la kwanza Januari 13, 2026 na amejionea mwenyewe kuwa maandalizi yamekamilika. “Tumeona maandalizi kwenye shule hii yamekamilika, kama ilivyo kwenye shule zote 18055 za msingi, hivyo natoa wito kwa wazazi wenye watoto walio na umri wa kuanza darasa la awali na la kwanza wawapeleke shuleni,” Prof. Shemdoe amesisitiza. Prof. Shemdoe amejionea madarasa ya awali mazuri ambayo yamejengwa kwa fedha za mapato ya n...

Prof Muhongo Aweka Mipango ya Uboreshaji wa Elimu Musoma Vijijini

UBORESHAJI WA ELIMU MUSOMA VIJIJINI  Utekelezaji ulenge haya: 1. Kuweka mbinu za kuongeza uelewa na upataji wa maarifa ya masomo yanayofundishwa wanafunzi wetu (improvement on levels of understanding and acquisition of knowledge (new?) by our pupils/students) 2. Kuweka mbinu za kuboresha ufaulu kwenye mitihani mbalimbali inayotolewa  (improvement on pupils'/students' performances in all examinations given to them) Wenye uzoefu wa masuala ya elimu na ajira wanaendelea kulalamikia "ufaulu" usioendana na "uelewa & maarifa"! Tusikate tamaa tuendelee kushughulikia hayo ya hapo juu. Asiwepo mtu wa kukaa pembeni na kuanza kulaumu wengine kwani sisi sote tunao wajibu wa kutekeleza yanayotuhusu ili kuleta mabadiliko! Kwa mfano: (i) Majukumu ya Mzazi Tunajua fika uwezo wa kiuchumi wa ndugu/jamaa zetu. Je, tunawasaidia au kuwawezesha wana ukoo wetu? (ii) Majukumu ya Jamii yenye shule: Tunaolaumu wengine, je sisi tunachangia uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na...

Cosmas Bulala Amefanya Kikao Kazi na CMT-Kwimba

*Kwimba -Mwanza* *Mbunge wa Jimbo la Kwimba na Mwanadiplomasia Mhe COSMAS BULALA ( MWANZA FINEST ) amefanya kikao kazi na wakuu wa idara  ( CMT ) wa halmashauri ya Kwimba na kuonyesha dira yake ya miaka mitano ( 2025-2030 ) ya ubunge wake.* *Mhe BULALA kawapongeza wataalamu wote Kwa KUENDELEA kuchapa kazi za kuwahudumia Wana Kwimba muda wote* *Wataalamu wote wamemshukuru Kwa kuzungumza nao na kumuahidi kushirikiana nae Mhe COSMAS BULALA ( MWANZA FINEST)* *Kwimba ni yetu sote tutaijenga Kwa pamoja🤝🤝🤝🤝*

Waziri Mkuu Aongoza Mkutano Kazi wa Mawaziri.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameongoza mkutano kazi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Serikali uliofanyika, Januari 12, 2026, katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina, jijini Dodoma. Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.