Prof Muhongo Aweka Mipango ya Uboreshaji wa Elimu Musoma Vijijini

GEORGE MARATO TV
0

UBORESHAJI WA ELIMU MUSOMA VIJIJINI 

Utekelezaji ulenge haya:

1. Kuweka mbinu za kuongeza uelewa na upataji wa maarifa ya masomo yanayofundishwa wanafunzi wetu

(improvement on levels of understanding and acquisition of knowledge (new?) by our pupils/students)

2. Kuweka mbinu za kuboresha ufaulu kwenye mitihani mbalimbali inayotolewa 

(improvement on pupils'/students' performances in all examinations given to them)

Wenye uzoefu wa masuala ya elimu na ajira wanaendelea kulalamikia "ufaulu" usioendana na "uelewa & maarifa"!

Tusikate tamaa tuendelee kushughulikia hayo ya hapo juu. Asiwepo mtu wa kukaa pembeni na kuanza kulaumu wengine kwani sisi sote tunao wajibu wa kutekeleza yanayotuhusu ili kuleta mabadiliko!

Kwa mfano:

(i) Majukumu ya Mzazi

Tunajua fika uwezo wa kiuchumi wa ndugu/jamaa zetu. Je, tunawasaidia au kuwawezesha wana ukoo wetu?

(ii) Majukumu ya Jamii yenye shule:

Tunaolaumu wengine, je sisi tunachangia uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwenye shule za nyumbani kwetu? Tunakaa pembeni, nani atufanyie kila kitu chenye manufaa ya watoto wa ndugu na jamaa zetu?

Tukajifunze kwa Wazaliwa wa Kijiji cha Butata! Wanaendelea kuchagia uboreshaji wa miundombinu ya elimu ya S/M Butata! Tulijenga Maktaba hapo!

Serikali ina wajibu wake, nasi tuna wajibu wetu! Tushirikiane na Serikali yetu kufanikisha matokeo mazuri ya elimu itolewayo kwenye shule za nyumbani kwetu!

Sospeter Muhongo 

13 Jan 2026

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top