Leo tarehe 13/1/2026 Rais wa jamuhuri ya Muungano wa tanzania amevunja rekodi kwa kuwa *Rais wa pili nchini tanzania* kufungua mkutano wa majaji na mahakama tangu mwaka 1984 ambapo *Hayati Mwl. Julius K nyerere* alihutubia mkutano huo.
Katika mkutano huo Rais samia ameiomba mahakama kuwa chombo huru na chenye utoaji wa haki kama ilivyoainishwa kwenye *ibara ya 107 na 107B* ya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia rais ameahidi kuwa serikali itaendelea kuuheshimu na kuulinda uhuru wa mahakama kama sheria za nchi zinavyotaka.
Rais samia amepasua mwamba kwa kuwaomba majaji na mahakimu kutendea haki watu, amesema *sio sahihi watu kuwekwa mahabusu au kufungwa kwa makosa ya kubambikiwa,* amewaomba majaji kuwa huru na kufanya kazi kwa kujipima ili kuondoa uonevu kwa watu wasio na hatia.
Rais samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya mahakama, mfano jengo la mahakama la pili kwa ukubwa zaidi barani afrika na la sita kwa ukubwa duniani la *Judiciary square* ni jengo lililojengwa jijini dodoma ambalo ndio makao makuu ya mahakama ya Tanzania. hivyo, rais ameahidi kuwa maboresho ya majengo hayo utaendelea siku hadi siku.
Rais samia amesema serikali imeimarisha mifumo ya kiteknolojia katika utaoaji haki, huu ni mfumo ambao haupo katika taifa lolote la afrika isipokuwa tanzania, hakika hilo ni jambo la kujivunia kama watanzania, nchi pekee yenye mfumo kama huu wa kisasa ni indonesia na nchi jirani zimekuwa zikija kujifunza tanzania. Hivyo kuanzia sasa ule msemo wa wansheria wa *”Justice delayed is justice denied”*(haki iliyochelewesha ni haki iliyopotea) tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuuzika rasmi kutokana na ufanisi wa mifumo mipya na ya kisasa katika mahakama zetu.
Rais samia amesisitiza pia kuna maboresho makubwa sana yamefanywa na serikali pale kwenye *shule ya sheria kwa vitendo (Law school of Tanzania)* kuwa leo ukienda pale law school huwezi kunanisha na miaka mitano iliyopita, na hii ni kweli kabisa kwa wale wakazi wa dar es salaam majengo na miundombinu iliyowekwa na serikali ya awamu ya sita haisimuliki.
Rais samia ameonyesha kwa vitendo dhamira *kazi na utu* kwa kuahidi kuwa mishahara ya watumishi wa mahakama wakiwemo majaji na mahakimu itapitiwa upya na kufanyiwa maboresho ili utu uonekane kwa vitendo katika majukumu yao.
Rais samia hajasita kabisa kusema kuwa atahakikisha mahakama za mwanzo zinafanyiwa matengenezo ili zifanane na hali ya kisasa kama ambavyo serikali imeboresha majengo ya vituo vya afya nchini kote, jambo hili litaongeza ari kwa mahakimu na watumishi wa mahakama kufanya kazi katika mazingira bora na yenye hadhi.
Rais samia amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kufanya kazi na muhimili wa mahakama, amewaomba kusimamia kiapo cha utumishi wa mahakama kwa manufaa ya umma na kusimamia utendaji haki kwa wananchi wa Tanzania.
#MamaAsemewe
#TanzaniaMoja



