Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kagera Waanza Kujinoa Kwa Bima ya Afya Kwa Wote

  Angela Sebastian ;Bukoba Viongozi wa sekta mbalimbali za Serikali,dini na watoa huduma za Afya mkoani Kagera wamejengewa uelewa juu ya utekelezaji wa sheria ya mfuko wa bima ya Afya kwa wote, ikiwa ni kuanza kutekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya siku 100 aliyoitoa wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Mafunzo hayo yametolewa leo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa kagera ambapo wamesisitizwa kutoea elimu juu ya sheria hiyo kwa nguvu zote kwa wananchi huku wahudumu wa Afya wakitakiwa kuondokana na mazoea katika utoaji wa huduma. Said Makola ni mratibu wa mpango wa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote  kutoka Wizara ya Afya akizungumza katika mafunzo hayo  alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya wanao wajibu wa kutoa miongozo na tafsiri ya sheria ya bima ya afya pamoja na kanuni zake ili ziweze kutekelezwa kwa urahisi katika mikoa yote Tanzania Bara. Alisema zaidi kaya laki  9.3 sawa na asilimia 23.7 kwa hawamu ya kwanza zimetambuliwa...

Serikali Kujenga Mtambo wa Kuchenjua Dhahabu Mwakitolyo Shinyanga

■ Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ▪️Zaidi ya tani 100 - 120 kuchenjuliwa kwa siku ■ Makundi ya vijana na wanawake kupatiwa leseni kupitia programu ya MBT ■ Leseni zisizoendelezwa kufutwa kwa mujibu wa sheria ■ Aelekeza Wachimbaji kufuata kanuni za usalama za uchimbaji kuepuka madhara *Mwakitolyo, Shinyanga Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* ya kuwasimamia wachimbaji wadogo, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ipo mbioni kuanza ujenzi wa mtambo wa kuchenjua madini ya dhahabu mkoani Shinyanga. Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Desemba, 2025 na Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde* alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na wachimbaji katika eneo la Mwakitolyo lililopo Shinyanga Vijijini. Waziri Mavunde alitangaza habari hizo njema kuwa, tayari Shirika la STAMICO limeanza utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais na kwamba eneo limeshapatikana katika Kijiji cha Mawemelu na ujenzi utaanza hivi karibuni. ...

Katibu Mkuu wa Ccm Afanya Mazungumzo na Balozi wa China

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Jumatatu, Desemba 22, 2025, amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China.

Dkt Mwigulu: Tuache Tabia ya Kuzoea Matatizo

*Afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Wilaya Nachingwea WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewaonya watendaji na watumishi wa umma waache tabia ya kuzoea matatizo hasa katika sehemu zinazotoa huduma kwa wananchi. Ametoa onyo hilo jana (Jumapili, Desemba 21, 2025) wakati akizungumza na wagonjwa na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali halisi ya utoaji huduma siku za wikiendi katika hospitali hiyo. Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ratiba ya kukagua ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, mara baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Ruangwa, aliamua kuanzia kwanza hospitalini kisha akaenda kwenye ukaguzi wa jengo hilo. Akiwa hospitalini hapo, alienda moja kwa moja kwenye chumba cha daktari wa zamu ili apate utaratibu wa kumhudumia mgonjwa pindi anapofika hospitalini na akaelezwa kwamba ni lazima mgonjwa aanzie mapokezi na kukata cheti ndipo aje kwa daktari. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikuta wagonjwa wawil...

Dkt.Mwigulu aagiza ziundwe timu za mikoa za wakaguzi wa miradi

_A watenge gharama ya vifaa vyataka_   WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemwagiza Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI) awaandikie barua Wakuu wote wa Mikoa ili waunde timu za majengo na miradi kwenye mikoa yao kama njia ya kuweka na wakandarasi wanaokiuka makadirio ya gharama za ujenzi (BOQ) wa miradi ya Serikali. "Yuko Mhandisi ambaye huwa anakagua miradi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru. Wakuu wa Mikoa wote wawe na timu za vijana wa aina hiyo, ili wasiuziwe mbuzi kwenye gunia. Iwe ni utamaduni wa Serikali kufanya mtihani wa aina hiyo," amesema Waziri Mkuu.  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Desemba 21, 2025) wakati.na viongozi na wananchi wa Wilaya Ruangwa na Nachingwea, mkoani Lindi akiwa katika ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo.   Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Waziri Mkuu amesema kuna baadhi ya miradi ambayo wakandarasi wake hawafuati BOQ. "Unakuta BOQ inataka nondo za mm 16 lakini mkan...

Waziri Simbachawene Awaomba Wana Kagera Kuwekeza Nyumbani

 Na Angela Sebastian; Bukoba Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Georgia Simbachawene amewataka wanakagera waishio nje ya Kagera kurudi nyumbai ili kuwekeza ikiwa ni kuasisi tamasha la Ijuka Omuka linalowakutanisha wanakagera wote kwa maslai ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Amesema hayo wakati wa kufunga Tamasha la utamaduni la Ijuka Omuka ambapo amewataka wazazi wote nchini kuwafundisha mila,desturi na utamaduni wa wazee wao ili waepuke kujiingiza katika mambo yasiyofaa. Aidha amewashauri wanakagera kufanya uzalishaji wa tija katika zao la ndizi na bidhaa nyingine zitokanazo na zao hilo pia kufanya utafiti wa ndizi zinazofaa kuzalishwa na kuzwpa nje ya nchi na kuingiza uchumi wa mkoa wa Kageta na Taifa letu  Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema lengo la Tamasha hilo ni kuirudisha Kagera kwenye uhalisia wake,kujadili maendeleo yao,kuibua fursa zilizopo na kutengeneza mikakati ya kutatua changamoto zinazoukabili wa mkoa huo.