Dkt.Mwigulu aagiza ziundwe timu za mikoa za wakaguzi wa miradi

GEORGE MARATO TV
0


_A watenge gharama ya vifaa vyataka_

 

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemwagiza Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI) awaandikie barua Wakuu wote wa Mikoa ili waunde timu za majengo na miradi kwenye mikoa yao kama njia ya kuweka na wakandarasi wanaokiuka makadirio ya gharama za ujenzi (BOQ) wa miradi ya Serikali.

"Yuko Mhandisi ambaye huwa anakagua miradi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru. Wakuu wa Mikoa wote wawe na timu za vijana wa aina hiyo, ili wasiuziwe mbuzi kwenye gunia. Iwe ni utamaduni wa Serikali kufanya mtihani wa aina hiyo," amesema Waziri Mkuu. 

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Desemba 21, 2025) wakati.na viongozi na wananchi wa Wilaya Ruangwa na Nachingwea, mkoani Lindi akiwa katika ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo.

 


Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Waziri Mkuu amesema kuna baadhi ya miradi ambayo wakandarasi wake hawafuati BOQ. "Unakuta BOQ inataka nondo za mm 16 lakini mkandarasi anaweka za mm 12. Kuna mahali zinatakiwa nondo sita, anaweka nondo nne. Jengo likikamilika, huwezi kuona na makubaliano ya BOQ. Nimeelekeza kila mkoa uwe na timu ya mazungumzo ya kukagua miradi ya Serikali."

"Mikoa yote wawe na vitengo hivi na wawe pia na vifaa vya majengo na miradi mingine badala ya kusubiri unaofanywa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru. Vitengo hivyo kazi yao ya kila siku nifuata mradi ili kubaini maeneo ambayo Serikali imetoa fedha na hazijatumika vizuri ili tuweze kuchukua hatua," amesisitiza.

 


Mapema, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Lindi-Ruangwa- Nachingwea uliojengwa kwenye kijiji cha Chimbila A wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.


Mradi huo chanzo chake kinatoka mito ya Nyangao na Chilua wilayani Lindi, unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wakati utakapokamilka, utanufaisha vijiji 56 katika Wilaya ya Ruangwa (vijiji 34), Wilaya ya Nachingwea (vijiji 21) na Wilaya ya Lindi (Kijiji 1). 

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa RUWASA, Mhandisi Walter Kirita amesema mradi huo unatarajiwa kugharimu sh. bill 119 na hadi sasa wameshalipa sh. bilioni 49 ujenzi wake umefikia asilimia 67 ya utekelezaji. 

Mradi huo umeanza kutekelezwa Februari, 2023 na awamu ya kwanza (Lot 1) ukamilifu kukamilika Juni, 2026. Hata hivyo, Mhandisi Kirita alimweleza Waziri Mkuu kwamba ifikapo Februari, 2026 baadhi ya vijiji vitaanza kupata huduma ya maji.



 baada ya kuweka jiwe la msingi, Dkt. Mwigulu alisema ameridhishwa na hatua ya utekelezaji mradi ambao umefikiwa. "Hivi ndivyo Rais Dkt. Samia anavyoona namna kazi inavyofanyika. Hapa tumeona malipo ya kutolewa ni kubwa kuliko fedha zilizo hadi sasa."

Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu mstaafu, Kassim M. Majaliwa kwa kuasisi mradi huo na kujifunza fedha za mradi kila mara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top