📌*Gharama nafuu yawa chachu ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.* 📌*Wizara ya Nishati yawapongeza* 📍Simiyu Jeshi la Magereza nchini limetekeleza agizo la Serikali la matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 suala linaloifanya jeshi hilo kujikinga na athari zinazotokana na nishati isiyo safi ya kupikia kama vile kuni na mkaa. Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi wa Ofisi za Magereza Mkoani Simiyu Bw. Simon Kotti , wakati wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia walipofanya ziara kwa lengo la kufuatilia miradi ya usambazaji wa Nishati Safi ya Kupikia na Teknolojia zake ikiwemo matumizi ya Rafiki Briquettes katika Magereza ili kubaini changamoto mbalimbali kama zipo. Kamishna msaidizi ameeleza kuwa kwa kuzingatia maelekezo ya agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye taasisi zinazolisha watu zaidi ya mia moja wao kama magereza walishalitekeleza hilo ili kujikinga na athari za matumizi ya ni...
Marato tv - Sauti ya Jamii