Waziri Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Ridhiwani Kikwete amesema serikali imefanikiwa kutoa vibari vya kazi elfu 41,500 za ajira katika mwaka 2025- 26 ikiwa ni sehemu ya kutambua umuhimu wa nguvu kazi katika ujenzi wa taifa la Tanzania.
Hayo amebainisha mapema hii leo Disemba 12, 2025 jijini dar es salaam, katika kikao kazi cha mkutano wa mawaziri na waandishi wa habari kilichoandaliwa na ofisi ya idara ya habari maelezo na kufanyika katika kituo cha urithi wa ukombozi ambapo amesema kwasasa serikali imetoa ajira elfu 12 huku ambapo nafasi elfu 7 ni kada ya afya na elfu 5 kwa kada ya elimu.
Aidha, Waziri Kikwete amesema kuwa serikali imejipanga kurahisisha zoezi la usahili kwa waombaji kuanzia awamu hii ambapo kwasasa kila muhusika atafanyiwa usahili katika mkoa wake jambo litakaloweza kuondoa usumbufu na ghalama kwa wahusika.
Katika kuboresha huduma wizara ya utumishi wa umma imefanikiwa kukamilisha marekebisho ya mfumo wa e-mrejesho utakaosaidia kukusanya taarifa za maoni na mapendekezo kwa wananchi ili kuweza kusaidia kuboresha huduma katika taaisisi pamoja na kuanzishwa kwa daftari la watumishi lenye lengo la kuwawezesha watumishi kutoa maoni au mapendekezo katika ofisi za serikali.
waziri Kikwete pia, amesema serikali haitamvumilia mtumishi yeyote wa umma anayefanya kazi kwa mazoea katika ofisi za serikali ambapo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.
Katika hatua nyingine, Waziri Kikwete amesema katika maerekezo ya dira ya taifa ya 2050, pamoja na msisitizo wa ilani ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza serikali kuongeza idadi ya ajira hadi kufikia milioni 8 lengo likiwa ni kuongeza fursa kwa vijana, kuongeza kipato kwa wananchi pamoja na kupunguza umaskini kwa watanzania.
Sambamba na hilo Waziri amesema kuwa kutokana na mkazo wa dira ya taifa ya 2050 juu ya matumizi ya kimtandao itasaidia kuchochea kasi ya matumizi ya kidigitali katika kuongeza hamasa ya kazi kwa watumishi katika kuwahudumia watanzania.
Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya idara ya habari maelezo, Zamaradi Kawawa amewataka watanzania kuchangamkia fursa za ajira zilizotolewa na serikali katika kujenga taifa la Tanzania kupitia sekta mbalimbali.






