Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jeshi la Magereza Latekeleza Agizo la Serikali la Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

📌*Gharama nafuu yawa chachu ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.* 📌*Wizara ya Nishati yawapongeza* 📍Simiyu Jeshi la Magereza nchini limetekeleza agizo la Serikali la matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 suala linaloifanya jeshi hilo kujikinga na athari zinazotokana na  nishati isiyo safi ya kupikia kama vile kuni na mkaa. Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi wa Ofisi za Magereza Mkoani Simiyu Bw. Simon Kotti , wakati wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia walipofanya ziara kwa lengo la kufuatilia miradi ya usambazaji wa Nishati Safi ya Kupikia na Teknolojia zake ikiwemo matumizi ya Rafiki Briquettes katika Magereza ili kubaini changamoto mbalimbali kama zipo. Kamishna msaidizi ameeleza kuwa kwa kuzingatia maelekezo ya agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye taasisi zinazolisha watu zaidi ya mia moja wao kama magereza walishalitekeleza hilo ili kujikinga na athari za matumizi ya ni...

Waziri Kikwete Aanika Mafanikio Makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita

 Waziri Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Ridhiwani Kikwete amesema serikali imefanikiwa kutoa vibari vya kazi elfu 41,500 za ajira katika mwaka 2025- 26 ikiwa ni sehemu ya kutambua umuhimu wa nguvu kazi katika ujenzi wa taifa la Tanzania.  Hayo amebainisha mapema hii leo Disemba 12, 2025 jijini dar es salaam, katika kikao kazi cha mkutano wa mawaziri na waandishi wa habari kilichoandaliwa na ofisi ya idara ya habari maelezo na kufanyika katika kituo cha urithi wa ukombozi ambapo  amesema kwasasa serikali imetoa ajira elfu 12 huku ambapo nafasi elfu 7 ni kada ya afya na elfu 5 kwa kada ya elimu. Aidha, Waziri Kikwete amesema kuwa serikali imejipanga kurahisisha zoezi la usahili kwa waombaji kuanzia awamu hii ambapo kwasasa kila muhusika atafanyiwa usahili katika mkoa wake jambo litakaloweza kuondoa usumbufu na ghalama kwa wahusika. Katika kuboresha huduma wizara ya utumishi wa umma imefanikiwa kukamilisha marekebisho ya mfumo wa e-mrejesho...

Ujenzi wa Jengo la Kituo Cha Mafunzo ya Kuongeza Thamani Madini ya Vito Waanza Jijini Arusha

■ Ni mkakati wa kuhakikisha madini vito yanaongezewa thamani nchini. ■Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais.Dkt. Samia katika kuendeleza mnyororo wa madini thamani. ■Waziri Mavunde amtaka mkandarasi kuongeza nguvukazi kukamilisha mradi kwa wakati. ▪️Atoa siku 7 kwa Katibu Mkuu kukutana na wakandarasi,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi. *Arusha* Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha mafunzo ya Uongezaji thamani madini ya vito kwa kuongeza nguvukazi na kufanya kazi kwa masaa 24 ili kukamilisha ujenzi wa jengo kwa muda mfupi. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 12, 2025 mkoani Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kituo hicho ulioanza ujenzi rasmi ambapo katika maelekezo yake amemtaka mkandarasi kuzingatia ujenzi bora wenye kukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali...

Waziri Ulega Atoa Agizo Kwa Kampuni ya Ujenzi ya Jasco ya Jijini Mwanza

 Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameutaka mkandarasi Jassie and Company (JASCO) kuhakikisha ujenzi wa Daraja la Mkuyuni unakamilika na kukabidhiwa ifikapo Januari 15, 2026, ili kupunguza adha wanayoipata wananchi hususan katika kipindi cha mvua. Ulega ametoa maelekezo hayo leo, Desemba 11, 2025, mkoani Mwanza wakati wa ziara maalum ya kukagua maendeleo ya mradi huo. Ziara hiyo imefanyika kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyemtaka Waziri kufika eneo hilo kubaini sababu za kuchelewa kwa utekelezaji wa ujenzi. Waziri Ulega amesema Serikali haitavumilia ucheleweshaji unaowaathiri wananchi na kusisitiza mkandarasi kuongeza kasi kuhakikisha daraja linakamilika kwa viwango vinavyostahili.

Askofu Mwamakula Amwaga Siri Kuhusu Jenista Mhagama

   *Ameandika Askofu Mwamakula* 🙏🙏🙏 Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama! Nusu ya pili ya mwaka 2023 ilikuwa na joto la aina yake katika siasa za Tanzania. Fenomena ijulikanayo kama Boniface Anyisile Mwabukusi ilianza kuchomoza na kung'ara katika siasa za Tanzania kupitia sakata la Mkataba wa Bandari. Mwabukusi, Dkt. Slaa na Mdude waliwekwa kizuizini kule Mbeya baada ya IGP kutangaza kuwa kuna watu walitaka kuipindua serikali ya Rais Samia. Askofu Mwamakula alijikuta akiwa katikati ya utetezi wa watu hao. Walitamkiwa makosa ya uhaini, lakini ghafla wakaachiwa wakiwa polisi bila ya kufikishwa mahakamani. Alphonce Lusako Mwamwile na mawakili wenzake walifungua kesi ya kupinga mkataba huo. Mwabukusi na wenzake wakawa mawakili wao. Lakini kesi ilitupwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa na jaji kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kuingilia mamlaka ya Bunge. Mwabukusi na wenzake kadhaa wakahamishia mapambano nje kwa kutangaza maandamano. Mwabukusi alianza kusakwa kama 'dhahabu ya Ch...

Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama!

 *Ameandika Askofu Mwamakula* 🙏🙏🙏 Usilolijua Kuhusu Jenista Mhagama! Nusu ya pili ya mwaka 2023 ilikuwa na joto la aina yake katika siasa za Tanzania. Fenomena ijulikanayo kama Boniface Anyisile Mwabukusi ilianza kuchomoza na kung'ara katika siasa za Tanzania kupitia sakata la Mkataba wa Bandari. Mwabukusi, Dkt. Slaa na Mdude waliwekwa kizuizini kule Mbeya baada ya IGP kutangaza kuwa kuna watu walitaka kuipindua serikali ya Rais Samia. Askofu Mwamakula alijikuta akiwa katikati ya utetezi wa watu hao. Walitamkiwa makosa ya uhaini, lakini ghafla wakaachiwa wakiwa polisi bila ya kufikishwa mahakamani. Alphonce Lusako Mwamwile na mawakili wenzake walifungua kesi ya kupinga mkataba huo. Mwabukusi na wenzake wakawa mawakili wao. Lakini kesi ilitupwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa na jaji kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kuingilia mamlaka ya Bunge. Mwabukusi na wenzake kadhaa wakahamishia mapambano nje kwa kutangaza maandamano. Mwabukusi alianza kusakwa kama 'dhahabu ya Chuny...