Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ulinzi wa Msitu wa Mgori Kuimarika

TFS kuongeza askari, vifaa na kujenga kituo cha walinzi Pohama Na Mwandishi Wetu, Singida Ulinzi wa Msitu wa Hifadhi wa Mgori mkoani Singida unatarajiwa kuimarika baada ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, kutangaza mpango wa kuongeza askari, kupeleka vifaa vya kisasa vya ulinzi na kuanzisha ujenzi wa Ranger Post katika kijiji cha Pohama. Profesa Silayo alitoa ahadi hiyo leo Jumanne, Novemba 11, 2025,  wakati wa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Singida, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Godwin Gondwe, kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa Msitu wa Mgori. Msitu huo, ambao ni miongoni mwa hifadhi muhimu nchini, umekuwa ukikabiliwa na changamoto za uchomaji moto, ukataji miti holela na uvamizi unaoathiri juhudi za Serikali katika kulinda rasilimali za misitu. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Gondwe alisisitiza umuhimu wa uhifadhi shirikishi, akipendek...

VERONICA MGETA AHIMIZA MSHIKAMANO WA KITAIFA

Alieyekua mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela Veronica Calist Mgeta katika hutuba yake mbele ya wandishi wa habari amesema kufuatia uungwaji mkono alioupata wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 Jimbo la Ilemela ni dhahiri kuwa anadeni kubwa kwa wanachi. “Imani yangu kwa wapiga kura ni kubwa namna mlivyojitokeza hakika ungwaji mkono huu sikua nautegemea hivi mmenipa heshima kubwa maishani mwangu najiona mwenye deni sina cha kuwalipa ila mungu pekee ndie anaweza kuwatosheleza alisema mgeta” Mgeta amesema kampeni zilizofanyika kata 19 za jimbo la ilemela zimeshuhudiwa   na wananchi  waliojitokeza kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni ili kutusikiliza sera mikakati ya kuwaleta maendeleo wananchi endapo CHAUMMA ingeshinda . Veronica alisema shukrani pekee hazitoshi ila ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuyafikia maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa jamii ya wana Ilemela wote kwa kuzingatia misingi ya utu na uzalendo. Aidha Veronica Mgeta amesema Uch...

Makusanyo ya Madini Simiyu Yavuka Malengo, Yafikia Zaidi ya Asilimia 103

📍Simiyu AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela, amesema mkoa huo umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Sekta ya Madini, ambapo makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 yamevuka malengo kwa kufikia zaidi ya asilimia 103 ya lengo lililowekwa kwa kipindi husika. Akizungumza mkoani Simiyu, Makolobela amesema kwa mwaka wa fedha uliopita, ofisi yake ilipewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 4, lakini walifanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 4.5.  “Kwa mwaka huu wa fedha tumewekewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 4.76, na hadi kufikia robo ya kwanza tayari tumekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 1.23, sawa na asilimia 103 ya lengo la robo mwaka,” amesema Makolobela. Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, makusanyo ya madini kupitia wachimbaji wadogo mkoani humo yamefikia zaidi ya Shilingi bilioni 17, hatua inayodhihirisha ukuaji na uimara wa sekta hiyo katika Mko...

Taju Yalaani Vikali Vurugu katika Kuhatarisha Amani

 Taasisi ya Tanzania Jumuishi (TAJU) imelaani vikali vitendo vya baadhi ya watu waliosababisha vurugu na kuharibu mali pamoja na kuikosesha amani jamii ya watu wenye ulemavu nchini. Hayo amebaisha mapema hii leo novemba 10, 2025, jijini Dar es salaam, Katibu wa Taasisi hiyo ya Tanzania Jumuishi (TAJU), Innocent Gabriel Siriwa, katika mkutano wa taasisi hiyo na vyombo vya habari  ambapo pia imevikumbusha vyama vya siasa na viongozi wa dini kutumia nafasi zao vizuri ili kulinda na kuhubiri amani nchini.  Aidha, Innocent  amesema (TAJU) Inapinga vikali  wote wanaounga mkono kwa kusema kuwa kudai haki kwa njia ya amani hakuwezi kufanikisha upatikanaji wa haki huku ikiwataka watanzania kufuta mtazamo huwo kwani hauna tija na ni wa wakati wa ukoloni Pia, amesema ili kulinda amani ya taifa la tanzania inapaswa watanzania kuacha kuiga mataifa madogo yanayofanya vurugu bila ufumbuzi wa matatizo ya kama Madagascar ikiwa pamoja na kutumia mitandao kuchagua mema na kuacha m...

SENDIGA AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU MANYARA* .

📌 *Majiko banifu 7,914 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku* .   📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200* . 📍 *MANYARA*  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Novemba 10, 2025 amezindua rasmi mradi wa kutuma na kutuma ujumbe kwa bei ya ruzuku mkoani Manyara. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wa kutafuta mkakati wa kitaifa wa kufikia na matumizi ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha,uzinduzi huu umefanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara iliyopo wilaya ya Babati, ambapo jumla ya majiko banifu 7,914 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya kiasi cha TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Sauti wakati wa Mheshimiwa, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kusaidia wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu. Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya yote mkoani Manyara ni kwa makini zo...

Waratibu wa Kitaifa wa Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu - Icglr Wakutana Jijini Kinshasa

Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Waratibu wa Kitaifa wa Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu  (ICGLR) umefanyika tarehe 10 Novemba, 2025 jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - DRC. Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje  (RIMC) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali (SUMMIT) wa Jumuiya hiyo iliyopangwa kufanyika Novemba 13 na 15, 2025 mtawalia. Mkutano huo umefunguliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketshi ambapo pamoja na masuala mengine, amewasihi waratibu hao kutumia mkutano huo kuja na mapendekezo yatakayoboresha utendaji kazi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu ili iweze kutekeleza kwa ufanisi zaidi majukumu yake ya msingi, ikiwemo kuleta amani, usalama na maendeleo katika nchi 12 Wanachama wa Jumuiya hiyo. Tanzania ikiwa moja ya nchi waasisi wa ICGL, inashiriki mkutano huo kikamilifu ambapo Mratibu wa Kitaifa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na...