Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

*Kasiki awapiga msasa wadau wa Sekta ya Madini* - *Abainisha fursa kubwa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani* - *Ajira zaongezeka mara tatu tangu 2018* MKURUGENZI wa Ukaguzi na Biashara ya Madini katika Tume ya Madini (MATD), CPA. Venance Kasiki, amewataka wadau wa Sekta ya Madini kuongeza ubunifu na ushiriki endelevu kwenye shughuli za uchumi wa madini kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazohitajika migodini badala ya kuendelea kuwa mawakala wa wazalishaji wa kigeni (OEMs). Akizungumza katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mjini Geita, Kasiki alisema ushiriki wenye tija unahitaji kampuni kuwa na mifumo madhubuti ya uendeshaji na usimamizi, kutoa bidhaa na huduma bora kwa wakati, kujifunza teknolojia mpya, pamoja na kushirikiana katika kuunda mitaji mikubwa ya pamoja. Alibainisha kuwa mnyororo wa thamani wa madini una fursa nyingi zinazoweza kushughulikiwa na Watanzania ikiwemo usambazaji wa mitambo ya migodini, huduma za TEHAMA, usafirishaji, fedha na bima, huduma za vyakula, vifaa kinga (PPE), famasia na vifaa tiba, ulinzi, uchorongaji, usafi na nyingine nyingi. “Ni wakati sasa kwa wadau wa sekta hii kutumia ipasavyo fursa zilizopo huku wakizingatia sheria na kanuni zilizowekwa, ili kuongeza tija kwa taifa,” alisisitiza Kasiki. Akizungumzia mchango wa sekta hiyo katika ajira, Kasiki alisema mwaka 2018 kulikuwa na ajira 6,668 kwa Watanzania na 335 kwa wageni. Hata hivyo, ifikapo mwaka 2024 idadi hiyo imeongezeka maradufu na kufikia zaidi ya Watanzania 19,371 na wageni 503. “Hii ni ishara tosha kuwa mchango wa Sekta ya Madini katika kutoa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa unaongezeka kwa kasi,” alisema. Hata hivyo, alitaja baadhi ya changamoto zinazoibuka kwenye zabuni na manunuzi kuwa ni pamoja na kutofuata taratibu za EOI na RFP, kuwepo kwa vigezo visivyo shindanishi vinavyolenga kampuni maalum, ushindani usio na tija kwa wazalishaji wa ndani, ubia usiokidhi matakwa ya kisheria na utoaji wa bidhaa au huduma zisizokidhi viwango. “Tume ya Madini itaendelea kusimamia Sheria ya Madini na Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania ili kuhakikisha sekta hii inawanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla,” aliongeza. Aidha, Kasiki aliwaasa Watanzania kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazotumika migodini katika eneo la Buzwagi mkoani Geita, ambapo Serikali imetenga eneo maalum kwa ajili ya uwekezaji huo.

 *Kasiki awapiga msasa wadau wa Sekta ya Madini* - *Abainisha fursa kubwa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani* - *Ajira zaongezeka mara tatu tangu 2018* MKURUGENZI wa Ukaguzi na Biashara ya Madini katika Tume ya Madini (MATD), CPA. Venance Kasiki, amewataka wadau wa Sekta ya Madini kuongeza ubunifu na ushiriki endelevu kwenye shughuli za uchumi wa madini kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazohitajika migodini badala ya kuendelea kuwa mawakala wa wazalishaji wa kigeni (OEMs). Akizungumza  katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mjini Geita, Kasiki alisema ushiriki wenye tija unahitaji kampuni kuwa na mifumo madhubuti ya uendeshaji na usimamizi, kutoa bidhaa na huduma bora kwa wakati, kujifunza teknolojia mpya, pamoja na kushirikiana katika kuunda mitaji mikubwa ya pamoja. Alibainisha kuwa mnyororo wa thamani wa madini una fursa nyingi zinazoweza kushughulikiwa na Watanzania ikiwemo usambazaji wa mitambo ya migodini, huduma za TEHAMA, ...

Rais Dkt Samia ampongeza Mwanariadha Simbu

*_Amkabidhi Nyumba jijini Dodoma*_ *_Mheshimiwa Majaliwa asema Simbu ameliheshimisha Taifa*_ *_Atoa zawadi kwa Timu zilizofanya vizuri kimataifa_*  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Alphonse Simbu kwa kuwa Bingwa wa Dunia wa mbio za marathon za Tokyo na kwamba ataendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ili itoe mchango zaidi katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza wigo wa upatikanaji ajira kwa vijana   Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi (Septemba 27, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla kuwapongeza wanamichezo na timu zilizofanya vizuri kwenye medani za kimataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kuwa, Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia amempatia Mwanariadha Simbu zawadi ya nyumba jijini Dodoma, sambamba na kikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 ikiwa ni ishara ya kutambua ushindi huo ambao u...

Glory wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Kawe awagusa watoto yatima Tegeta Kibo

Katika kufanya Kampeni za nyumba kwa nyumba, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Glory Tausi Shayo alipata neema ya kualikwa kama Mgeni rasmi katika Maulid iliyofanyika katika Kituo cha Watoto yatima cha Almarkaz kilichopo Tegeta Kibo  Maulid hiyo imefanyika leo Jumamosi ya tarehe 27/09/2025, ikihudhuriwa na wakazi wa maeneo mbalimbali, hasa wa jirani na kituo hicho.  Bi. Tausi alipata wasaa wa kuwasilisha misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho, aliyochangiwa na wasamaria wema

Kila jiwe lina thamani - Keraka

Geita MJIOLOJIA kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Godfrey Keraka, amesema kuwa kila jiwe lina thamani kwa sababu ya mchango katika sekta ya madini, maendeleo ya taifa na teknolojia ya kisasa duniani. Maoni kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Keraka ameeleza kuwa sekta ya madini inachangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) na ni urithi muhimu wa nchi unaopaswa kulindwa. Ame mfano wa madini ya kitu kama Amethyst, Rose-Quartz na Quartz ambayo hutumika kutengeneza mapambo ya thamani, wakati madini ya chuma yanahusishwa zaidi na ujenzi wa ushirika, ushirika wa magari, meli na mashine mbalimbali. Aidha, shaba hutumika kwenye nyaya za umeme, feldspar kwenye vigae na mapambo, na pyrite kwenye mbolea, mapambo pamoja na rasilimali wa tindikali ya salfyuriki. Kwa upande mwingine, makaa ya mawe yatajwa kuwa chanzo muhimu cha nishati, huku dhahabu na fedha zikibainishwa kama madini yenye thamani yanayotumika katika hifadhi ya fedha, ...

Mirerani Mines Officer Commends Mining Commission at Geita Gold Fair

Geita  The Resident Mines Officer for Mirerani, George B. Kaseza, has praised the Mining Commission for its effective participation at the ongoing Geita Gold Fair 2025, taking place at the Dr. Samia Suluhu Hassan Grounds in Bombambili, Geita. During his visit to the Commission’s pavilion, Mr. Kaseza commended the level of preparation, noting that the exhibitions showcased the Commission’s commitment to creating awareness about Tanzania’s mineral sector.  He encouraged Tanzanians to take an active role in the sector, highlighting the numerous opportunities available in mineral exploration, value addition, and trade. Mr. Kaseza emphasized that broader participation from local investors and stakeholders would strengthen the country’s economy and ensure Tanzanians benefit more from the nation’s mineral wealth. The Geita Gold Fair 2025, which runs from September 18 to 28, has brought together stakeholders from across the mining industry to promote investment, innovation, and collab...

Kila Jiwe Lina Thamani – Keraka

Geita MJIOLOJIA kutoka Ofisi ya  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Godfrey Keraka, amesema kuwa kila jiwe lina thamani kwa sababu ya mchango wake katika sekta ya madini, maendeleo ya taifa na teknolojia ya kisasa duniani. Akizungumza kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Keraka ameeleza kuwa sekta ya madini inachangia  asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) na ni urithi muhimu wa nchi unaopaswa kulindwa. Ametolea mfano wa madini ya vito kama Amethyst, Rose-Quartz na Quartz ambayo hutumika kutengeneza mapambo ya thamani, wakati madini ya chuma yanahusishwa zaidi na ujenzi wa miundombinu, utengenezaji wa magari, meli na mashine mbalimbali. Aidha, shaba hutumika kwenye nyaya za umeme, feldspar kwenye vigae na mapambo, na pyrite kwenye mbolea, mapambo pamoja na uzalishaji wa tindikali ya salfyuriki. Kwa upande mwingine, makaa ya mawe yametajwa kuwa chanzo muhimu cha nishati, huku dhahabu na fedha zikibainishwa kama madini yenye thamani ku...