Akizungumza kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Keraka ameeleza kuwa sekta ya madini inachangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) na ni
Ametolea mfano wa madini ya vito kama Amethyst, Rose-Quartz na Quartz ambayo hutumika kutengeneza mapambo ya thamani, wakati madini ya chuma yanahusishwa zaidi na ujenzi wa miundombinu, utengenezaji wa magari, meli na mashine mbalimbali. Aidha, shaba hutumika kwenye nyaya za umeme, feldspar kwenye vigae na mapambo, na pyrite kwenye mbolea, mapambo pamoja na uzalishaji wa tindikali ya salfyuriki.
Kwa upande mwingine, makaa ya mawe yametajwa kuwa chanzo muhimu cha nishati, huku dhahabu na fedha zikibainishwa kama madini yenye thamani kubwa yanayotumika katika hifadhi ya fedha, mapambo, sarafu na vifaa vya kielektroniki.
Keraka pia amesisitiza umuhimu wa graphite na lithium kama madini ya kimkakati katika utengenezaji wa betri na mifumo ya kuhifadhi nishati.
“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kila jiwe lina thamani kubwa. Miamba na madini ni urithi wa taifa unaopaswa kulindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Keraka.