Katika kufanya Kampeni za nyumba kwa nyumba, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Glory Tausi Shayo alipata neema ya kualikwa kama Mgeni rasmi katika Maulid iliyofanyika katika Kituo cha Watoto yatima cha Almarkaz kilichopo Tegeta Kibo
Maulid hiyo imefanyika leo Jumamosi ya tarehe 27/09/2025, ikihudhuriwa na wakazi wa maeneo mbalimbali, hasa wa jirani na kituo hicho.
Bi. Tausi alipata wasaa wa kuwasilisha misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho, aliyochangiwa na wasamaria wema