Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Daktari Samia Suluhu yajayo yanafurahisha wilaya ya Mbinga

Mgombea Urais Kwa tiketi ya CCM Dokta SAMIA SULUHU HASSAN ambae pia ni mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Taifa Leo September 21-2025 amefanya mkutano wa Kampeni eneo la viwanja vya Sun city, Kata ya Mbinga mjini B, katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Dokta SAMIA SULUHU HASSAN, akiwahutubia maelfu ya wananchi wa wilaya ya Mbinga katika mkutano huo wa Kampeni wa kihistoria, amewaomba wanambinga ifikapo oktoba 29 wakichague chama Cha Mapinduzi CCM na kukumbuka ngazi ya Urais, wabunge, na madiwani Ili wasimamie vyema mzuri wa ILANI ya uchaguzi wa CCM wa mwaka 20025/20. Mama SAMIA SULUHU HASSAN, Akifurahishwa na mapokezi makubwa ya upendo wa wananchi wa wilaya ya Mbinga ameahidi wakimchagua oktoba 29 na kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ataendeleza Uboreshaji wa huduma za afya, Elimu, umeme, mawasiliano, mawasiliano, mageuzi ya kilimo na usalama wa chakula. Upande wa ujumbe wa ubunge Jimbo la Mbinga mjini Ndugu Jonas MBUNDA na ubunge Jimbo la Mbinga vijini Ndugu JUDITH KAPINGA w...

Oktoba 29 Hakuna Nywiinywii,Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Vimejipanga-Dkt Samia

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama chama Mapinduzi (CCM)Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Pemba wasikubali kuchokozeka wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu. Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye viwanja vya Gombani ya kale wilayani Chakechake Pemba,Dkt.Samia ambaye ni Rais anayemaliza awamu ya kwanza ya yongozi wake, amesisitiza kuwa serikali yake itahakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa usalama. Amesema wakati huu wapo watu wanaokitumia kipindi hiki kuchokoza wengine hivyo wao kamwe wasikubali kuchokozeka. Dkt.Samia amesema yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama, hivyo anawahakikishia Watanzania kuilinda nchi. Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,Serikali imejitahidi sana kusimamia utulivu wa kisiasa,usalama na amani ndani ya nchi. ‘’Napenda kuongeza sauti yangu kwenye masuala ya ulinzi na usalama,ndani ya miaka mitano yote hamjasikia pepepe,mkisikia basi ni ajali imetokea ,wameku...

Waziri Dk Stergomena Tax azungumza na bodaboda

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax,  tarehe 20 Septemba 2025, alikutana na kufanya Kikao na Viongozi wa Maafisa usafirishaji kwa njia ya Pikipiki (Bodaboda) wakiwawakilisha kundi kubwa la Bodaboda Wilaya Magu mkoani Mwaanza,  Kikao ambacho kimetokana na maombi ya mara kwa mara ya Viongozi wa Bodaboda kuomba miadi ya kukukutana na kuzungumza na Waziri Dkt. Tax. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya Magu ndugu Fratha Andrea Katumwa. Baada ya kusikiliza changamoto za Maafisa usafirishaji hao, Dkt Tax amewapongeza kwa umoja wao na kuahidi kushirikiana na Uongozi wa Wilaya Magu kuzitatua changamoto hizo haraka iwezekanavyo ili kuwapunguzia adha hizo ikiwemo uanzishwaji wa SACOS ya Bodaboda Magu. Aidha, ametoa wito kwa Viongozi hao kuwahamasisha wafuasi wao kujitokeza kwenda kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba 2025 ili kutumia haki yao ya Kikatiba. Akihitimisha, Waziri wa...

Waziri Mkuu Majaliwa Kufungua Maonesho Ya Madini Geita

Shoo awataka wadau kujifunza teknolojia mpya za uchimbaji Geita, Septemba 21, 2025 Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Geita yanatarajiwa kuzinduliwa kesho na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita. Akizungumza leo, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Samwel Shoo, amesema Tume ya Madini inashiriki maonesho hayo kwa mara ya nane mfululizo na imeandaa huduma za elimu kwa wadau wote wa sekta ya madini watakaotembelea mabanda yake. Elimu hiyo itahusu teknolojia za kisasa za utafiti, uchimbaji na uchenjuaji wa madini. “Huu ni msimu muhimu unaowaunganisha wachimbaji, wachenjuaji, wafanyabiashara na wadau wengine wa madini ili kubadilishana ujuzi na kujifunza mbinu mpya. Pia ni nafasi ya kuimarisha uhusiano wa sekta ya madini na sekta nyingine za kijamii na kiuchumi,” amesema Shoo. Ameongeza kuwa ni fursa kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na wawekezaji kujifunza teknolojia mbalimbali zinazotumika k...

Makonda ashindwa kujizuia, amwaga machozi madhabahuni

Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametokwa machozi wakati wa maombi katika Huduma ya Radio Safina lililopo Mbauda jijini Arusha  Makonda alijikuta kwenye hali hiyo I wakati alipopewa nafasi kusalimia kanisani hapo leo Jumamosi 20, 2025 akisema nia yake katika kuwania nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi wa Arusha. Amesema kufanya hivyo ni kutimiza kusudi la Mungu lililopo ndani yake huku akiwaomba waumini kumuombea ashinde awe mbunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.  Amesema Taifa linahitaji viongozi ambao watatimiza kusudi la Mungu hapa duniani, wenye maono na wasiotanguliza maslahi binafsi badala yake watekeleza matakwa ya waliowachagua kuwa kwenye mamlaka

Rais Samia anatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuendeleza maarifa - Majaliwa

  *_Asema elimu haiwezi kukamilika kama hakuna maadili._*   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kwa dhati mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo BAKWATA na wadau wote wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuleta mshikamano wa kitaifa kupitia elimu.    Amesema kuwa elimu haiwezi kukamilika kama hakuna maadili kwani ndiyo yanayojenga utu, heshima na mshikamano wa kijamii. "Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu inakuza maarifa na ujuzi, sambamba na malezi yanayoimarisha tabia bora na maadili ya kizalendo kwa vijana wa Kitanzania". Amesema hayo Jumamosi Septemba 20, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia katika hafla ya usiku ya utoaji tuzo za elimu za mufti iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serena hotel jijini Dar es Salaam. "Rais Dkt. Samia anawapongeza sana BAKWATA kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika masuala yote ya maendeleo ya jamii hususan mchango wenu ka...