Daktari Samia Suluhu yajayo yanafurahisha wilaya ya Mbinga

GEORGE MARATO TV
0

Mgombea Urais Kwa tiketi ya CCM Dokta SAMIA SULUHU HASSAN ambae pia ni mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Taifa Leo September 21-2025 amefanya mkutano wa Kampeni eneo la viwanja vya Sun city, Kata ya Mbinga mjini B, katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga,


Dokta SAMIA SULUHU HASSAN, akiwahutubia maelfu ya wananchi wa wilaya ya Mbinga katika mkutano huo wa Kampeni wa kihistoria, amewaomba wanambinga ifikapo oktoba 29 wakichague chama Cha Mapinduzi CCM na kukumbuka ngazi ya Urais, wabunge, na madiwani Ili wasimamie vyema mzuri wa ILANI ya uchaguzi wa CCM wa mwaka 20025/20.


Mama SAMIA SULUHU HASSAN, Akifurahishwa na mapokezi makubwa ya upendo wa wananchi wa wilaya ya Mbinga ameahidi wakimchagua oktoba 29 na kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ataendeleza Uboreshaji wa huduma za afya, Elimu, umeme, mawasiliano, mawasiliano, mageuzi ya kilimo na usalama wa chakula.


Upande wa ujumbe wa ubunge Jimbo la Mbinga mjini Ndugu Jonas MBUNDA na ubunge Jimbo la Mbinga vijini Ndugu JUDITH KAPINGA wameishukuru serikali ya chama Cha Mapinduzi-CCM Kwa utekelezaji mzuri wa ILANI ya uchaguzi wa mwaka 2020/2025 nakuwaomba wananchi wa majimbo yote mawili kukichagua chama Cha Mapinduzi na taaluma yake wilaya ili kuunda Dola la kuunda Serikali ya Maendeleo.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top