Oktoba 29 Hakuna Nywiinywii,Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Vimejipanga-Dkt Samia

GEORGE MARATO TV
0



 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama chama Mapinduzi (CCM)Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Pemba wasikubali kuchokozeka wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye viwanja vya Gombani ya kale wilayani Chakechake Pemba,Dkt.Samia ambaye ni Rais anayemaliza awamu ya kwanza ya yongozi wake, amesisitiza kuwa serikali yake itahakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa usalama.

Amesema wakati huu wapo watu wanaokitumia kipindi hiki kuchokoza wengine hivyo wao kamwe wasikubali kuchokozeka.

Dkt.Samia amesema yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama, hivyo anawahakikishia Watanzania kuilinda nchi.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,Serikali imejitahidi sana kusimamia utulivu wa kisiasa,usalama na amani ndani ya nchi.

‘’Napenda kuongeza sauti yangu kwenye masuala ya ulinzi na usalama,ndani ya miaka mitano yote hamjasikia pepepe,mkisikia basi ni ajali imetokea ,wamekufa wangapi na labda mtu mwenyewe atakwenda kuchokoza na kuvunja amani,lakini hamjasikia vurugu ndani ya nchi hii.Hata wale waliovuka mpaka na kuleta vurugu ndani ya nchi yetu tuliwashughulikia na hawajathubutu kurudi tena”alisema Dkt.Samia na kuongeza kuwa

‘’Niwaombe sana ndugu zangu,kipindi hiki ni kipindi ambacho wengine wanakitumia kuchokozana,niwaombe msichokozeke,kuweni kama mimi mama yenu,dada yenu,bibi yenu na ndugu yenu nachokozwa sana,lakini sichokozeki hivyo niwaombe sana msichokozeke’’

Amewahimiza watanzania kutokubali kuvunja amani ya nchi kwa sababu ya uchaguzi.

‘’Tusivunje amani kwa sababu ya uchaguzi,hapana.Akiumia mmoja imeumia familia,familia yote itahangaika kupeleka vyakula hospitali na kurudi,fedha za dawa,tusichokozeke,tusiende kuvunja amani kwa sababu ya uchaguzi’’ameonya

‘’Sisi wote ni wamoja,mfano mimi nina usuli pia Pemba kwa hiyo sitafurahi kuona ndugu yangu iwe makunduchi au Pemba kapigwa au kuumiza sitakubali,kwa hiyo niwaombe wote tutunze amani na utulivu,tunapochokozwa tusichokozeke’’amesisitiza

Ameendelea kuwatoa hofu watanzania kwa kuwahakikishia kuwa wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 mwaka huu hakutakuwa na vurugu na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura.

‘’Niwahakikishie vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuilinda nchi yetu,mimi ndiye Amiri Jeshi Mkuu,Tumejinga vyema kuilinda nchi yetu kwa hiyo hakutakuwa na nywii wala nywinywinywi,tokeni,amshaneni nendeni mkapige kura’’ameahidi

Ameongeza ‘’Wenzetu wanayolalamikia hakuna lisilozungumzika.Tutakaa,tutazungumza,tusiende kuleta vurugu kuvunja amani kwa sababu hili halikufanyika,Tukapige kura,turudi nyumbani tusubiri matokeo’’

Ameahidi kufanya makubwa zaidi kwa miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi endapo watapewa tena ridhaa kuwa Marais.

Amewaahidi wananchi wa pemba kujenga kiwanja cha ndege chenye hadhi cha kimataifa,kuikamilisha barabara ya chake-mkoani,kujenga bandari ya wete itakayojengwa kwa fedha za mkopo kutoka korea.

Ameahidi pia kujenga na kukamilisha barabara saba ndani ya pemba na kusisitiza kuwa fedha za kutekeleza miradi hiyo zipo. 









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top