Makonda ashindwa kujizuia, amwaga machozi madhabahuni

GEORGE MARATO TV
0

Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametokwa machozi wakati wa maombi katika Huduma ya Radio Safina lililopo Mbauda jijini Arusha 

Makonda alijikuta kwenye hali hiyo I wakati alipopewa nafasi kusalimia kanisani hapo leo Jumamosi 20, 2025 akisema nia yake katika kuwania nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi wa Arusha.

Amesema kufanya hivyo ni kutimiza kusudi la Mungu lililopo ndani yake huku akiwaomba waumini kumuombea ashinde awe mbunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. 

Amesema Taifa linahitaji viongozi ambao watatimiza kusudi la Mungu hapa duniani, wenye maono na wasiotanguliza maslahi binafsi badala yake watekeleza matakwa ya waliowachagua kuwa kwenye mamlaka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top