Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Msimtarajie Akawa Samia Huyu Baada ya Uchaguzi Mkuu!

George Michael Uledi. September 16,2025! Siku ile nikiwa natembea zangu mitaani mara Naliona ujumbe ukinijia kichwani mwangu,ulikuja kwa njia ya neno(suati) ukisema 👇🏿👇🏿👇🏿 "Nenda kawaambie,Samia huyu HATOKUWA yule tena baada ya Uchaguzi Mkuu huu 2025...mkajiandae.."!.. Jana nikiwa kwenye gari ya Kaka yangu Mh Paul Douglas Mwakajumba tukitoka kwenye ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi Wilayani Kyela,eneo la Ipinda Kyela,ambako Mh Spika alikuwa ndiye mgeni RASMI,mara gafla Kaka yangu Paul Deoglas Mwakajumba akasema...; "....watu wengi watashangaa,Samia huyu HATOKUWA huyu baada ya Uchaguzi Mkuu...." Nilistuka!👆👆kwani alichokisema Kaka yangu Paul ni kile kile ambacho Mungu alinipitishia kichwani mwangu kwa sauti miezi mitatu nyuma! Kichwa changu kikawa tayari "kimetiki" Unabii ule bila hata KUMWAMBIA Kaka Paul kwamba I saw the same,back days! Hakika Nawaambia👇🏿👇🏿 I.Ole wenu mnayedhania Mama huyu ni DHAIFU!She is about to prove you wrong,very...

Mtoto wa Familia ya Baba wa Taifa Alaani Vikali Polisi Kushambualia Wafuasi wa Chadema

 Tukio la maafisa wa Jeshi la Polisi kuwashambulia na kuwapiga baadhi ya viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamefika kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Wakili Tundu Lissu leo, Jumatatu Septemba 15.2025 limeendelea kulaaniwa na wadau mbalimbali Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mkurugenzi Mwenza wa Gazeti la Jamhuri Manyerere Jackton naye amelaani vikali tukio hilo, ambapo ameeleza uchungu uliopo kuona Jeshi la Polisi linageuka chombo cha mateso kwa raia wasiokuwa na hatia, tena wakifanyiwa ukatili wakiwa kwenye viunga vya Mahakama  Amesema maafisa wa Jeshi la Polisi wanapaswa kufahamu kuwa wao ni sehemu ya jamii, na kwamba haikubaliki kuona wakitumia nguvu kuwapiga ndugu na jamaa zao, kama sio Watanzania wenzao Manyerere amesema Tanzania kama Taifa, linapaswa kufahamu kuwa kukandamizwa kwa sauti ya wana...

Sagini Ampigia Kampeni Dkt Samia,Madiwani na Dkt Mahera Awe Mbunge Butiama

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini amehudhuria Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama ambapo amemnadi na kumuombea kura za ndio Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Dkt. Wilson Charles Mahera. Mhe. Sagini ameeleza kuwa kuna kila sababu ya mwananchi wa Butiama kumpa kura ya ndio Mgombea wa urais, ubunge na udiwani anayetokana na Chama Cha Mapinduzi ili kutengeneza muunganiko wa mafiga matatu ambayo yatarahisha kuleta maendeleo kama yalivyopatika katika kipindi chake cha 2020-2025. "Kipindi cha Mwaka 2020 Wilaya ya Butiama tuliongoza kutoa kura nyingi za Rais Mwaka 2025 tunaye Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Wilson Mahera pamoja na madiwani wa Kata zote 18 wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi msifanye kosa wapeni kura nyingi za ndio ili wanapoongea lugha moja maendeleo yanajaa ndani ya Butiama kwani Mhe. Rais Samia ni mtu wa huruma na nyie ni mashuhuda hatukua...

Wasira: Ujenzi Wa Reli Utafufua Uchumi, Kuneemesha Wakulima

Na MWANDISHI WETU  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kufufuliwa kwa Reli ya TAZARA, ujenzi wa reli ya kusini Mtwara -Mbamba bay) utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa mikoab ya Kusini na NyandA za Juu Kusini. Amesema ujenzi wa reli hizo ambao upo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 na kuboreshwa kwa sekta ya kilkmo, kutasaidia kuleta ahueni kubwa ya kiuchumi kwa wakulima hususan wa mkoani Njombe. Wasira ameeleza hayo leo Septemba 15, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kutoka kata 37 zilizo katika majimbo matatu ya Wilaya ya Njombe mkoni Njombe. "Kwa miaka mitano ijayo Rais Samia (Rais Dk. Samia Suluhu Hassan) amesaini mkataba na Zambia na China kufufua reli ya TAZARA ambayo inapita Makambako. Reli ya TAZARA itaunganisha maeneo haya na Uwanja wa Ndege wa Songwe na Bandari ya Dar es Salaam na ilikusudiwa hivyo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere kwamba tupitishe hii reli kwa sababu kilimo hiki kitaleta mizigo ya kw...

Dkt.Nchimbi Aomba Wananchi Handeni Kuichagua Ccm Kwa Kura Nyingi Ili Ishinde Kwa Kishindo Uchaguzi Mkuu

MGOMBEA Urais mwenza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dkt. Emmanuel  Nchimbi amewaomba wananchi wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kukipigia kura Chama hicho ili kishinde kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025. Ametoa ombi hilo alipokuwa akihutubia maelfu ya Wananchi waliofika kumsikiliza,katika uwanja wa Kigoda leo Septemba 15, 2025 wilayani Handeni ambapo ameendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura za mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan,wabunge na madiwani. Dkt.Nchimbi ameanza siku yake ya kwanza  mkoani Tanga kufanya mikutano yake ya kampeni za  Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025,na mpaka sasa tayari ameshafanya mikutano yake ya kampeni ndani ya mikoa 11 mpaka sasa.