Na MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kufufuliwa kwa Reli ya TAZARA, ujenzi wa reli ya kusini Mtwara -Mbamba bay) utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa mikoab ya Kusini na NyandA za Juu Kusini.
Amesema ujenzi wa reli hizo ambao upo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 na kuboreshwa kwa sekta ya kilkmo, kutasaidia kuleta ahueni kubwa ya kiuchumi kwa wakulima hususan wa mkoani Njombe.
Wasira ameeleza hayo leo Septemba 15, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kutoka kata 37 zilizo katika majimbo matatu ya Wilaya ya Njombe mkoni Njombe.
"Kwa miaka mitano ijayo Rais Samia (Rais Dk. Samia Suluhu Hassan) amesaini mkataba na Zambia na China kufufua reli ya TAZARA ambayo inapita Makambako. Reli ya TAZARA itaunganisha maeneo haya na Uwanja wa Ndege wa Songwe na Bandari ya Dar es Salaam na ilikusudiwa hivyo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere kwamba tupitishe hii reli kwa sababu kilimo hiki kitaleta mizigo ya kwenda bandarini.
"Pia tunajenga reli nyingine kwa ajili ya watu wa Mtwara kwenda Mbamba bay na tunaunganisha reli kutoka katikati ya Mtwara na Mamba bay kuja Rudewa kwa ajili ya kuchukua chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya Nchuchuma, huwezi kubeba chuma kwa lori, lazima tubebe chuma kwa reli tuunganishe Rudewa na bandari ya Mtwara halafu unaiunganisha na dunia.
Alieleza kuwa, kwa kufanya hivyo maana yake ni kwamba kwa miaka mitano serikali itakayoundwa na CCM italeta mabadiliko makubwa kwa maisha ya wakulima kwa sababu itakuwa imewafikishia mazao yao sokoni kwa urahisi.
Aidha ndg. Wasira ametumia mkutano huo kumwombea kura mgombea urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan naWasira: Ujenzi Wa Reli Utafufua Uchumi, Kuneemesha Wakulima wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama katika uchaguzi Mkuu mnamo tarehe 29 oktoba 2025.