📌 *Majiko banifu 9,330 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mbeya* 📌 *Wilaya Sita kunufaika na mradi* 📌 *Kila Wilaya pata majiko 1,555* 📍 *MBEYA* Serikali ya Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu, Rodrick Mpogolo leo Jumanne Septemba 2, 2025 imepokea mradi wa kusimamia na matumizi ya majiko banifu 9,330 yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mradi Mhandisi wa miradi kutoka kwa nishaji vijijini (REA), Raya Majallah amesema, Kupitia utafiti 2016 unakadiria kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya kila mwaka huu ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini Tanzania, kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba ya upikaji kwa kutumia matumizi yasiyo safi na salama. Hivyo kwa kutambua hilo, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijiji imeaanda mpango wa kuamua na kuondoa majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku ili kupona athari za kiafya na mazingira zinazotoka...
Marato tv - Sauti ya Jamii