Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika, Godfrey Ng’urah Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Aprili 11, 2025.

Mabalozi Kutangaza Utalii wa Tanzania Kimataifa

📌*Ziara ya utalii ya Mabalozi kuchochea ushirikiano wa Tanzania na mataifa mengine* *Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa ziara ya  Mabalozi ya kutembelea vivutio vya utalii  vilivyopo Zanzibar pamoja na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 11, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika uzinduzi na ufunguzi wa ziara ya Waheshimiwa Mabalozi ya katika vivutio vya utalii. “ Tanzania ni sehemu nzuri ya utalii duniani na ni imani yangu kuwa mtapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa duniani kwa wapanda milima, lakini  pia tuna hifadhi ya wanyama ya Serengeti, Ngorongoro na sehemu zingine,” amesema Dkt. Biteko. Ameongeza “ Mtatembelea pi...

Jaji Mtungi-hakuna Chama cha Siasa cha Kuzuia Uchaguzi Mkuu Mwaka huu

Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema hata kama kauli ya ‘No reform, no Election’ haijavunji sheria ya vyama vya siasa,lakini kamwe isitumike kama kichocheo cha kuvunja sheria za nchi na katiba ya  Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Amesema ofisi yangu inafuatia kwa karibu kauli kama hizo zinazotumiwa na baadhi ya vyama vya siasa katika kuvunja sheria na katiba ya nchi. Jaji, Mutungi amesema hayo wakati akizungumza na George Marato Tv huku akisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa chenye uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwaka huu 2025. Amesema katika mazungumzo yake na waandishi wahabari baada ya kushiriki warsha ya wadau wa kujadili namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu 2025,akiwaeleza wazi mazungumzo yake na vyama vya siasa ikiwemo Chadema kwamba ofisi yake hauwezi kuvumilia kauli zinazolenga kuvunja sheria za nchi. Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa ndani, CHADEMA wamekuwa wakieleza kuwa, bila mabadiliko katik...

Robbi Samwelly Awakumbusha Wazazi Malezi Bora Kwa Watoto Kwenye Kongamano

Na Shomari Binda-Butiama  MJUMBE wa Baraza la UWT Taifa kutoka mkoa wa Mara na mkurugenzi wa kituo cha malezi ya watoto wa kike cha nyumba salama Robbi Samwelly amewakumbusha wazazi kuzingatia malezi bora ya watoto. Ukumbusho huo ameutoa leo aprili 9,2025 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya wazazi kwa mkoa wa Mara. Akizungumza kwenye kongamano la madhimisho hayo kwenye ukumbi wa Kanisa Katoriki Butiama amesema kama malezi yatasimamiwa vizuri kuanzia ngazi ya jamii vitendo vya ukatili havita kuwepo. Amesema kituo cha nyumba salama kimekuwa mstari wa mbele kuwapokea watoto wa kike wanaokimbia na wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na kuomba kuwepo kwa usimamizi Nora wa malezi. Robbi amesema kila mmoja akitimiza jukumu lake kwenye suala la malezi hakuna mtoto atakayekimbia nyumbani kutikana na kuogopa kufanyiwa ukatili. Mjumbe huyo amesema kupitia kituo cha nyumba salama kilichopo Butiama na Serengeti wameweza kuwalea watoto kwa kuwaps elimu hadi kufikia ngazi ya chuo kikuu. Mwenyek...

Ccm Yafungua Milango ya Kugombea Nafasi za Dola

 

Wakandarasi Jimbo la Tarime Vijijini Waonyeshwa Maeneo ya Ujenzi wa Miradi 19 Fedha za Csr

Na Shomari Binda-Tarime WAKANDARASI wanaokusudiwa kutekeleza miradi 19 ya maendeleo kwenye vijiji mbalimbali kwenye jimno la Tarime Vijijini wameonyeshwa maeneo ya utekelezaji. Ziara iliyofanyika april 9,2025 iliyowahusisha wataalam na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini imeshiriki huku lengo ikiwa kuanza utekelezaji wake mara moja. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mbunge imesema maeneo yaliyofikiwa ni pamoja na Nyarokoba Kijiji cha Msenge ambapo kuna ujenzi wa jengo la utawala shule ya msingi Musege pamoja na nyumba ya mwalimu. Eneo la pili lililofikiwa ni Kata ya Gorong'a Kijiji cha Kenyamsabi ambapo kuna ukamilishwaji wa zahanati ya Kijiji hicho pamoja na Kijiji cha Nyanungu ambapo pia kuna ujenzi wa zahanati. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka ofisi ya mbunge Kata ya Itiryo Kijiji cha Kangariani pia kimefikiwa kikiwa na ujenzi wa nyumba ya mtumishi na zahanati. Ujenzi wa jengo la kufulia na njia za kupita wagonjwa kituo cha afya Magoma Kijiji cha Magoma kimefikiwa n...