Na Shomari Binda-Butiama
MJUMBE wa Baraza la UWT Taifa kutoka mkoa wa Mara na mkurugenzi wa kituo cha malezi ya watoto wa kike cha nyumba salama Robbi Samwelly amewakumbusha wazazi kuzingatia malezi bora ya watoto.
Ukumbusho huo ameutoa leo aprili 9,2025 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya wazazi kwa mkoa wa Mara.
Akizungumza kwenye kongamano la madhimisho hayo kwenye ukumbi wa Kanisa Katoriki Butiama amesema kama malezi yatasimamiwa vizuri kuanzia ngazi ya jamii vitendo vya ukatili havita kuwepo.
Amesema kituo cha nyumba salama kimekuwa mstari wa mbele kuwapokea watoto wa kike wanaokimbia na wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na kuomba kuwepo kwa usimamizi Nora wa malezi.
Robbi amesema kila mmoja akitimiza jukumu lake kwenye suala la malezi hakuna mtoto atakayekimbia nyumbani kutikana na kuogopa kufanyiwa ukatili.
Mjumbe huyo amesema kupitia kituo cha nyumba salama kilichopo Butiama na Serengeti wameweza kuwalea watoto kwa kuwaps elimu hadi kufikia ngazi ya chuo kikuu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Fadhil Maganya ambaye alikuwa mgenj rasmi kwenye maadhimisho hayo amewataka viongozi wa jumuiya hiyo ngazi zote kusimamia suala la maadili ya watoto.
Amesema jumuiya hiyo ndiyo yenye jukumu la kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata elimu
Katika maadhimisho hayo limefsnyika kongmsno lililojadili maadili,elimu,malezi pamoja na utunzaji wa mazingira.





Comments
Post a Comment