Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dk. Machar chini ya kizuizi cha nyumbani katikati ya mvutano unaoongezeka

Vikosi vya usalama vya Nchini Sudan Kusini vimemweka Makamu wa Kwanza wa Rais na kiongozi wa upinzani Dk. Riek Machar Pamoja na Mkewe Angelina Teny ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani katika kizuizi cha nyumbani huko Juba huku kukiwa na mvutano wa kisiasa unaozidi kutokota na hivyo kuzua hofu na wasiwasi wa kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sudan Kusini imekuwa na amani rasmi tangu makubaliano ya 2018 yalipomaliza mzozo wa miaka mitano kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na Machar, ambao ulisababisha Mauaji ya karibu watu 400,000.  Hata hivyo, uhusiano kati ya viongozi hao wawili, ambao wametawala siasa za Sudan Kusini kwa miongo kadhaa, bado ni mbaya. Kuzuiliwa nyumbani kwa Dk. Riek Machar kunaonekana kuhatarisha makubaliano ya amani. Reath Muoch Tang, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya SPLM-IO, aliiambia Redio Tamazuj kwamba barua iliyotangaza kuzuiwa nyumbani kwa Machar iliwasilishwa na maafisa wakuu wa usalama, akiwemo Waziri wa Ulinzi Jeneral...

Serikali Yaja na Mkakati wa Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogo Kufikia Uwekezaji Mkubwa wa Madini

▪️ *Waziri Mavunde aelekeza kuwepo na mpango maalum wa kuwatambua wachimbaji wanaofanya vizuri* ▪️ *Mfuko wa Dhamana wa Wizara ya Fedha kutumika kuongeza mtaji kwa wachimbaji* ▪️ *STAMICO yapewa jukumu kuongeza vifaa zaidi vya Utafiti wa madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo* ▪️ *Wachimbaji waandaa maandamano makubwa kumpongeza Rais Samia* 📍 *Dodoma* Waziri wa Madini Mhe.  Anthony Mavunde ameeleza ķuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imekuja mkakati maalum wa kuwawezesha Wachimbaji Wadogo kupiga hatua zaidi na kufaulu na hatimaye kumiliki migodi mikubwa kupitia mpango maalum utakaorahisisha upatikanaji wa mitaji, teknolojia ya kisasa, na kuwajengea uwezo endelevu wa uchimbaji na kibiashara.  Amebainisha hayo leo Machi 27, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano maalum na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za u...

Shamira Achangia Madirisha 13 Ujenzi Nyumba ya Mtumishi Kusini Unguja

 Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa Zanzibar kwenye muendelezo wa ziara yake amefanya zoezi la ukaguzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Katika ziara yake hio ya Mkoani Kusini Unguja ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya Katibu na kuchangia madirisha 13 kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja  inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Phidelis D. Phidelis. Akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi nyumba hio ya katibu wa UVCCM mkoa wa ambayo iko katika hatua za mwisho. Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake. “Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itaenda kupunguza baadhi ya gharama ambazo Jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi Mtendaji wetu wa vijana mkoa wa Kusini Unguja, pia sasa itakuwa ni rahisi kwa Jumuiya kujua ni wapi tunaweza kumpata Mtendaji wetu kwa haraka zaidi”. Ameong...

Ccm Mara Kugawa Kadi za Kielektroniki 645,000 Kwa Wanachama Wake Kuanzia Machi 29, 2025

Na Shomari Binda-Musoma CHAMA cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara kimepanga kugawa kadi za kielekronicki kwa wanachama wake 645,000 kuanzia machi 29. KATIBU wa Siasa, Uenezi,Itikadi na Mafunzo Mkoa wa Mara Simon George Rubugu amesema kuwa Chama hicho kimepokea kadi za wanachama wa mkoa huo waliosajiliwa kwa mfumo wa  Kielektroniki zipatazo  645,000 ambapo kinatarajia kuanza zoezi la ugawaji wa kadi hizo. Rubugu ameyasema hayo leo Machi 27,  2025, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake.  Amesema kadi hizo zimebooreshwa kisasa  huku  akitoa  msisitizo kwa wanachama wa CCM  ambao bado hawajasajiliwa kujisajili kwani zoezi hilo ni endelevu.  Kiongozi huyo amesema idadi ya kadi hizo  ni zaidi ya asilimia 51 ya makisio ya wapiga kura na zitasaidia kuwatambua wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya matawi, Kata, Wilaya hadi Mkoa kabla ya kuingia katika uchaguzi  unaotarajia kufanyika mwaka huu. "Kadi hizi zitakuwa ...

Wanawake 3,000 Mkoa Wa Dodoma Kupata Mafunzo Ya Veta-Rc Rosemary

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Mkoa wa Dodoma, kinatarajia kutoa mafunzo kwa kundi la ‘Wanawake na Samia’ wapatao 3000 linalounga mkono matamanio ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta Usawa wa kijamii na kijinsia ambayo ni kufikia mwaka 2030, ifike 50 kwa 50 kwa kila kundi kupata haki sawa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akifungua mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kwa ajili ya kundi la Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, zitakazotolewa kwa kundi hilo na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) tawi la Jijini Dodoma. *“Mhe. Dkt Samia amekua akitamani kila kundi la Mtanzania lipate haki sawa ndio maana anasema hataachwa mtu nyuma awe ni mwanamke, mtu? mwenye ulemavu, mzee, kijana au mtoto. Anatamani Wanawake wa Tanzania washike uchumi sawa na wanaume, Makundi maalum ambayo yapo nyuma yashike uchumi sawa na makundi mengine”.* Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, amekipongeza Chuo cha VETA Dodoma kwa kuandaa mafunzo hayo amba...

Majaliwa Aagiza: Serikali inatoa Fedha, Simamieni Manunuzi ya Dawa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie vema fedha za ununuzi wa dawa zinazotolewa na Serikali na kuhakikisha zahanati na vituo vyote vya afya vina dawa za kutosha ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Amesema Serikali inatenga fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa muhimu kote nchini hivyo hatarajii kuona mwananchi anakwenda kupata huduma kisha anaambiwa akanunue dawa kwenye maduka yaliyoko nje ya vituo vya afya au zahanati. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika (Machi 25, 2025) katika uwanja wa Shule ya Sekondari Kiraweni, Tarafa ya Usangi, wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro akiwa katika ziara ya siku moja ya kukagua miradi wilayani humo. "Sitarajii mwana-Mwanga ameenda zahanati, kituo cha afya au hospitali ya Wilaya anaandikiwa cheti na mganga, halafu unamwambia nenda kwenye duka la mtu binafsi ukanunue, wakati dawa hiyo inapatikana kituoni hapo.” Amesema Serikali inatoa fedha nyingi kwa...