Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yaja na Mkakati wa Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogo Kufikia Uwekezaji Mkubwa wa Madini


▪️ *Waziri Mavunde aelekeza kuwepo na mpango maalum wa kuwatambua wachimbaji wanaofanya vizuri*

▪️ *Mfuko wa Dhamana wa Wizara ya Fedha kutumika kuongeza mtaji kwa wachimbaji*

▪️ *STAMICO yapewa jukumu kuongeza vifaa zaidi vya Utafiti wa madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo*

▪️ *Wachimbaji waandaa maandamano makubwa kumpongeza Rais Samia*


📍 *Dodoma*

Waziri wa Madini Mhe.  Anthony Mavunde ameeleza ķuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imekuja mkakati maalum wa kuwawezesha Wachimbaji Wadogo kupiga hatua zaidi na kufaulu na hatimaye kumiliki migodi mikubwa kupitia mpango maalum utakaorahisisha upatikanaji wa mitaji, teknolojia ya kisasa, na kuwajengea uwezo endelevu wa uchimbaji na kibiashara. 

Amebainisha hayo leo Machi 27, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano maalum na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla.

Waziri Mavunde, amesema kuwa mpango huo utasaidia Wachimbaji Wadogo kupiga hatua na kuwa Wachimbaji wa Kati, hatimaye kuwa wamiliki wa migodi mikubwa inayochangia kikamilifu katika Pato la Taifa na uchumi kwaujumla.

✅️ *Waziri Mavunde Aelekeza Kuwepo na Mpango Maalum wa Kuwatambua Wachimbaji Wanaofanya Vizuri*

Mhe. Mavunde amewaelekeza watendaji wa Wizara kupitia Tume ya Madini kuandaa mfumo wa kutambua Wachimbaji Wadogo wanaofanya vizuri katika shughuli za uchimbaji ili waingie kwenye mpango maalum wa kuwawezesha kwa awamu hatimaye kupiga hatua na kuona manufaa ya uchimbaji wao.

“Sote tunafahamu mchango wa Wachimbaji Wadogo katika maduhuli ya Serikali, hivyo tunataka kuona wachimbaji wadogo wanakuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wakubwa. Tunatengeneza mfumo wa kuwatambua wale wenye bidii, weledi, katika sekta ili kuwawezesha hadi kufikia hatua ya kumiliki migodi mikubwa, tunataka miaka michache ijayo kuwepo na mabilionea Wakitanzania waliotokana na Sekta hii” amesema Waziri Mavunde.


✅️ *Mfuko wa Dhamana wa Wizara ya Fedha Kutumika Kuongeza Mtaji kwa Wachimbaji*

Waziri Mavunde amesema kuwa, ktika mkakati huo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, itatumia Mfuko wa Dhamana wa Serikali (Export Guarantee Scheme) ambao utatumika kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mikopo nafuu ili wawezekuendesha shughuli zao ikiwemo kununua mitambo na vifaa vya kisasa vya uchimbaji na kwamba hatua hiyo inalenga kuwatoa Wachimbaji Wadogo kutoka katika uchimbaji wa majaribio na kuwapeleka katika uchimbaji wa kisasa wenye tija zaidi.

“Tunataka kuwapa wachimbaji wadogo uwezo wa kumiliki mitambo bora ili waongeze uzalishaji na kuongeza mapato yao. Kupitia mfuko wa dhamana, wachimbaji wataweza kupata mikopo yenye masharti nafuu ambayo itawawezesha kuwekeza zaidi kwenye sekta ya madini,” amesisitiza Waziri Mavunde.


✅️ *STAMICO Yapewa Jukumu la Kuongeza Vifaa vya Utafiti wa Madini kwa Ajili ya Wachimbaji Wadogo*

Aidha, Katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanapata taarifa sahihi za maeneo yenye madini kabla ya kuanza uchimbaji, Waziri Mavunde ameliagiza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao ni walezi wa Wachimbaji Wadogo jukumu la kuongeza vifaa vya kWadogombali na mashine za uchorongaji (Rig Machine) na kuwa STAMICO inatakiwa kuhakikisha Wachimbaji Wadogo wanapata huduma za kisasa kwa gharama nafuu ili kuwawezesha kufanya uchimbaji wa kitaalamu na wenye ufanisi.

“Zile rig zikija hatutagawa kwanza mpaka tutakapoongeza na vifaa vya kisasa ili wachimbaji wadogo wasiwe wanachimba tu bali na kuweza kuchakata madini yao kwa wakati huohuo. Tunataka wachimbaji wapate huduma bora kwa gharama nafuu, na hii itaongeza uzalishaji wao kwa kiwango kikubwa,”  ameongeza Waziri Mavunde.


✅️ *Wachimbaji Waandaa Maandamano Makubwa Kumpongeza Rais Samia*

Katika hatua nyingine, Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini kupitia Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) wamepanga kufanya maandamano makubwa ya amani kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuboresha mazingira ya wachimbaji wadogo.

Rais wa FEMATA, John Bina, amesema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani, sekta ya madini imekuwa na mageuzi makubwa ambayo yamewanufaisha wachimbaji wadogo kwa kiwango kikubwa.

“Tumeona namna Serikali ya Mama Samia inavyowajali wachimbaji wadogo. Tumepewa mitaji nafuu, taratibu za leseni zimeboreshwa, na sasa tunapewa nafasi ya kumiliki migodi mikubwa. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, na tutafanya maandamano ya kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya katika sekta ya madini na kumuonyesha kuwa wachimbaji tunamuunga mkono,” amesema Bina.

Kwa juhudi hizi, wachimbaji wadogo wana matumaini makubwa ya kupiga hatua na kuwa sehemu muhimu ya wawekezaji wakubwa katika sekta ya madini nchini Tanzania. Serikali imeonyesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanapata fursa sawa na wawekezaji wakubwa, jambo linalotarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta hiyo na uchumi wa taifa kwa ujumla.


✅️ *Serikali Kuendelea Kushirikisha Makundi ya Wachimbaji Wote Bila Ubaguzi*

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amesema kuwa Serikali inajivunia mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo katika mnyororo mzima wa sekta ya madini, kwani wao ni wadau muhimu wanaochangia ukuaji wa sekta hiyo na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kushirikisha makundi yote ya wachimbaji bila ubaguzi, kwa kuhakikisha wanapata fursa ya kutoa maoni yao juu ya changamoto wanazokabiliana nazo, pamoja na kupendekeza njia bora za kuimarisha sekta. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa sera, sheria, na taratibu zinazowekwa zinaakisi mahitaji halisi ya wadau wa Sekta ya Madini, wakiwemo wachimbaji wadogo, ili kuwezesha ukuaji endelevu wa sekta hiyo.







Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...