Shamira Achangia Madirisha 13 Ujenzi Nyumba ya Mtumishi Kusini Unguja

GEORGE MARATO TV
0


 Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa Zanzibar kwenye muendelezo wa ziara yake amefanya zoezi la ukaguzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Katika ziara yake hio ya Mkoani Kusini Unguja ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya Katibu na kuchangia madirisha 13 kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja  inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Phidelis D. Phidelis.

Akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi nyumba hio ya katibu wa UVCCM mkoa wa ambayo iko katika hatua za mwisho. Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.



“Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itaenda kupunguza baadhi ya gharama ambazo Jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi Mtendaji wetu wa vijana mkoa wa Kusini Unguja, pia sasa itakuwa ni rahisi kwa Jumuiya kujua ni wapi tunaweza kumpata Mtendaji wetu kwa haraka zaidi”. Ameongeza Mshangama









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top