Vikosi vya usalama vya Nchini Sudan Kusini vimemweka Makamu wa Kwanza wa Rais na kiongozi wa upinzani Dk. Riek Machar Pamoja na Mkewe Angelina Teny ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani katika kizuizi cha nyumbani huko Juba huku kukiwa na mvutano wa kisiasa unaozidi kutokota na hivyo kuzua hofu na wasiwasi wa kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sudan Kusini imekuwa na amani rasmi tangu makubaliano ya 2018 yalipomaliza mzozo wa miaka mitano kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na Machar, ambao ulisababisha Mauaji ya karibu watu 400,000. Hata hivyo, uhusiano kati ya viongozi hao wawili, ambao wametawala siasa za Sudan Kusini kwa miongo kadhaa, bado ni mbaya. Kuzuiliwa nyumbani kwa Dk. Riek Machar kunaonekana kuhatarisha makubaliano ya amani. Reath Muoch Tang, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya SPLM-IO, aliiambia Redio Tamazuj kwamba barua iliyotangaza kuzuiwa nyumbani kwa Machar iliwasilishwa na maafisa wakuu wa usalama, akiwemo Waziri wa Ulinzi Jeneral...
Marato tv - Sauti ya Jamii