Na Shomari Binda-Musoma WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wa Kata za Mwisenge,Kamnyonge na Makoko wamemuomba mbunge la jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kugombea tena uchaguzi mkuu wa 2025 muda ukifika. Kauli hizo wamezitoa leo februari 3 kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya mbunge huyo kuelezea utekelezaji wa ilani kwenye kipindi cha 2020/2025. Wamesema hawana sababu za kutomchagua tena muda ukifika kwa kuwa kile alichokifanya katika utekelezaji wa ilani kinaonekana kwa macho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzj ( CCM) Kata ya Kamnyonge Emanuel Bwimbo na baadhi ya wajumbe wamesema kwenye kikao chao kinachowafanya kumuomba mbunge huyo kugombea ni kazi zake zinazoonekana. Bwimbo amesema Kata ya Kamnyonge katika huduma za afya leo wananchi hawaangaiki wakiwa na zahanati inayotoa huduma bora na hawawezi kuangaika na maneno ÿa wapita njia. " Wajumbe naomba mthibitishe mbele ya mbunge na diwani wetu kama mtawachagua tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 muda...
Marato tv - Sauti ya Jamii