Na Shomari Binda-Musoma
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wa Kata za Mwisenge,Kamnyonge na Makoko wamemuomba mbunge la jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kugombea tena uchaguzi mkuu wa 2025 muda ukifika.
Kauli hizo wamezitoa leo februari 3 kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya mbunge huyo kuelezea utekelezaji wa ilani kwenye kipindi cha 2020/2025.
Wamesema hawana sababu za kutomchagua tena muda ukifika kwa kuwa kile alichokifanya katika utekelezaji wa ilani kinaonekana kwa macho
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzj ( CCM) Kata ya Kamnyonge Emanuel Bwimbo na baadhi ya wajumbe wamesema kwenye kikao chao kinachowafanya kumuomba mbunge huyo kugombea ni kazi zake zinazoonekana.
Bwimbo amesema Kata ya Kamnyonge katika huduma za afya leo wananchi hawaangaiki wakiwa na zahanati inayotoa huduma bora na hawawezi kuangaika na maneno ÿa wapita njia.
" Wajumbe naomba mthibitishe mbele ya mbunge na diwani wetu kama mtawachagua tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 muda ukifika",amesema.
Kwa kujibu kauli za Mwenyekiti huyo wajumbe wa Kata ya Kamnyonge kwa pamoja wamesema wana imani na mbunge na diwani wao na kuwaomba kugombea tena.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kata ya Mwisenge Mnyugu Mnyugu amesema wao walishaamua na kutangaza mapema kwenda na mbunge Mathayo kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Wenyeviti wa chama na serikali za mitaa ya Kata ya Makoko wamesema wao wamefunguliwa Kata yao kwenye elimu,afya na hata miundombinu hivyo hawawezi kuwaacha mbunge na diwani wao.
Diwani wa Kata ya Makoko na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema kazi zilizofanywa zinaonekana na kwa kutambua walichokifanya.
Akizungumza kwenye mikutano ya Kata hizo mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema bado ataendelea kuwapigania wananchi wa Musoma mjini na hawezi kukatishwa tamaa.
Amesema leo amebakiza kupambana kuona wananchi wanakuwa na uchumi mzuri na kuwa na fedha mfukoni baada ya miradi mingi kutekelezwa.

.jpg)




Comments
Post a Comment