Leo Machi 3, 2025 Bodi ya ithibati imezindiliwa rasmi katika hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika , Tawi la Tanzania Bwana Edwin Soko amesema kuwa kuzinduliwa Kwa Bodi ya Ithibati ni mwelekeo chanya wa ukuaji wa sekta ya habari Nchini Tanzania.
Soko amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi ya Ithinati ya Waandishi wa Habari na kuweka bayana kuwa, Kwa sasa taaluma ya habari inakwenda kuheshimika kama zilivyo taaluma nyingine hapa Nchini hivyo Bodi hiyo itasaidia kulinda maadili ya uandishi wa habari Tanzania.
Soko ameongeza kuwa , MISA TAN inahimiza waandishi wote Nchini kubadilika kimtazamo ili kuendama na mabadiliko ya sasa hasa Kwa kufanya kazi Kwa weledi Kwa kuwa tayari Kuna chombo kinacho ratibu mwenendo wa taaluma ya habari.
Hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ithinati ya waandishi wa habari ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Labudi katika hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam

.jpg)

Comments
Post a Comment