Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Sare za Jwtz zamponza, afungwa Jela Miezi Sita

Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya  kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa. Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 07.01.2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka,  mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 huko kijiji cha Kasisa, wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhi...

Tanzania na Uingereza Kushirikiana Katika Kuendeleza Madini Mkakati

▪️Waziri Mavunde ainisha Mkakati wa uongezaji thamani Madini ▪️Taasisi za Jiolojia na Utafiti Madini  za Tanzania na Uingereza kushirikiana ▪️Watanzania kujengewa uwezo kukuza ujuzi 📍Dar es Salaam Serikali ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye sekta ya madini hususani katika kujengea uwezo watu wake, kubadilishana uzoefu, uongezaji thamani madini na kuwekeza kwenye kufanya tafiti mbalimbali ili kukuza sekta ya madini na kupanua mnyororo wa thamani ili kuongeza ajira na kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa. Hayo, yameelezwa Jana na Waziri wa Madini, *Mhe. Anthony Mavunde* katika ofisi ndogo za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, *Mhe. Marianne Young*. "Kwanza kabisa *Mhe. Balozi Young* amefika ofisini kujitambulisha kwakuwa ana muda mfupi nchini tangu awasili lakini pia tumezungumzia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Uingereza. Katika mazungumzo hayo...

Bashungwa awakutanisha Polisi na Latra kujadili Mikakati ya Kuzuia ajali za Barabarani

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameongoza kikao kilichoikutanisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kujadili na kuweka mikakati ya kuzuia ajali za barabarani nchini. Kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi ya kuongeza mikakati ya kuzuia ajali zinazosababishwa na makosa ya uzembe. Pamoja na mambo mengine, wamejadili utaratibu wa utoaji wa leseni kwa madereva pamoja na kuweka mikakati ya pamoja kwa Jeshi la Polisi na LATRA ya kupambana na kuzuia ajali za barabarani. Kikao hicho kimefanyika Dodoma, leo Januari 06, 2025 ambapo kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura na Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa barabara (LATRA), DCP Jo...

Mheshimiwa Simbachawene akabidhi Gari la Wagonjwa Mtera

   Mtera:  🗓️ 07/01/2025.     📍Ikiwa takribani siku  42 zimepita ambazo ni sawa na mwezi mmoja na siku kumi na mbili lilipofanyika zoezi la ufungaji wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba leo hii wananchi hao wa Kata ya Mtera wamefanikiwa kukabidhiwa gari hilo la kubebea wagonjwa  Akikabidhi gari hilo Mheshimiwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Mb) wa Jimbo la Kibakwe Mheshimiwa George B.Simbachawene mbele ya viongozi wengne wa serikali Mheshimiwa Simbachawene amesisitiza kulitunza gari hilo ili liweze kuwa msaada kwa wananchi hao hasa akina mama wajawazito ambao wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kutoweza kukimbizwa haraka katika kituo Cha afya kwaajili ya kupewa huduma ya kujifungua.   Naye diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Robert Maulya amemshukuru Mheshimiwa Simbachawene ambae kwa Umoja wake yeye na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania Dkt Samia Suluhu Hass...

Vijana Mnaotaka Kuoa Mc Pilipili atoa Ushauri Kwa Vijana

-Mc Pilipili: Usioe Mwanamke Mwenye Tamaa Mchekeshaji / Mchungaji maarufu  hapa Tanzania  na Afrika Mashariki nzima Mc pilipili amefunguka ukweli mzima kuwa yeye na Mama wa mtoto wake hawapo sawa kabisa na kuwapa ushauri vijana wanaotaka kuingia kwenye ndoa. "Nazani nilioa mwanamke asiyekuwa na upendo wa kweli na aliyejaa Tamaa sana za maisha mazuri  ndoa maana amekuwa akinisumbua sana. Ushauri  ni jambo la bure vijana wenzangu tutafute wanawake wasiokuwa na Tamaa"- Amezungumza Mc Pilipili.

Rais wa zamani wa Ufaransa afikishwa mahakamani akituhumiwa kupokea pesa kutoka kwa Gaddafi

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amefikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, kwa tuhuma za kupokea mamilioni ya euro za ufadhili usio halali katika kampeni za kugombea urais 2007, kutoka kwa hayati Rais wa Libya Muammar Gadaffi. Sarkozy amekuwa akikana mashtaka hayo na kesi hiyo itaendelea kwa muda wa miezi mitatu. Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha kihafidhina anakabiliwa na mashtaka ya "kuficha ubadhirifu wa fedha za umma, ufisadi, ufadhili haramu wa kampeni na njama ya kufanya uhalifu," imesema ofisi ya mwendesha mashtaka wa fedha. Waendesha mashitaka wanasema mwaka 2005, Sarkozy, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa wakati huo, aliafikiana na Gaddafi, ili kupata ufadhili wa kampeni ili kuiunga mkono serikali yake katika uwanja wa kimataifa ambapo ilikuwa imetengwa. Gaddafi aliyeondolewa madarakani kisha kuuawa mwaka 2011. Wachunguzi wanadai alifanya mapatano ya kifisadi na serikali ya Libya, yaliyohusisha majasusi wa Libya, gaidi aliyepatikana na hatia...