Mtera:
🗓️ 07/01/2025.
📍Ikiwa takribani siku 42 zimepita ambazo ni sawa na mwezi mmoja na siku kumi na mbili lilipofanyika zoezi la ufungaji wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba leo hii wananchi hao wa Kata ya Mtera wamefanikiwa kukabidhiwa gari hilo la kubebea wagonjwa
Akikabidhi gari hilo Mheshimiwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Mb) wa Jimbo la Kibakwe Mheshimiwa George B.Simbachawene mbele ya viongozi wengne wa serikali Mheshimiwa Simbachawene amesisitiza kulitunza gari hilo ili liweze kuwa msaada kwa wananchi hao hasa akina mama wajawazito ambao wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kutoweza kukimbizwa haraka katika kituo Cha afya kwaajili ya kupewa huduma ya kujifungua.
Katika makabidhiano hayo ya gari wameweza kufika viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mpwapwa akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Mwanahamisi Ally.
Imetolewa na:
Afisa habari wa Jimbo la Kibakwe
07/01/2025