Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jeshi la polisi wilaya ya musoma latambua mchango wa mbunge Mathayo

Na Shomari Binda-Musoma JESHI la Polisi Wilaya ya Musoma limetambua mchango uliotolewa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kufanikisha mashindano ya Polisi Jamii Cup 2024. Kabla ya kuanza mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 20 mbunge huyo alitoa ng'ombe kama zawadi kwa bingwa na mipira 16. Cheti cha pongezi cha kutambua mchango huo kimetolewa jana septemba 29 na mgeni rasmi wa fainali ya mashindano hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi Nenrad Sindano Amesema wanatambua mchango wa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo na moyo wake wa upendo na kujitoa katika masuala ya kijamii. Sindano amesema lengo la mashindano hayo limefanikiwa kwa kuwa elimu juu ya utoaji wa taarifa juu ya uhalifu na wahalifu ikiwemo ushiriki wa uchaguzi wa serikali za mitaa ilitolewa. Amesema vijana na wote waliopsta elimu kupitia mashindano hayo wanapaswa kuishi nayo na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo. " Mashindano yetu yamemalizika salama uju...

Rais wa mpito wa Burkina faso aimarisha upatikanaji wa huduma za afya maeneo ya vijijini

Rais wa mpito wa Burkina faso kapteni  Ibrahim Traoré amekabidhi magari kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwenye vijiji visivyokuwa na Hospitali. Magari hayo ambayo ni Hospitali zinazotembea yamekabidhiwa kwa wizara ya afya yakiwa na vifaa tiba vya kisasa pamoja na vitanda vya wagonjwa, Fridge za dawa, Mitungi ya gesi na Jenereta za Umeme.  Kapteni Traoré ambaye ameliongoza Taifa la Burkina faso tangu septemba 30 mwaka 2022 amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya,elimu pamoja na usalama wa raia na Mali zao. Kiongozi huyo pia tayari amezifutia leseni za uchimbaji wa madini makampuni yote ya kigeni.  Amechukua hatua hiyo baada ya kubaini Taifa hilo halinufaiki na madini yanayochimbwa na makampuni ya kigeni ambapo kwa sasa shughuli za uchimbaji madini nchini humo zinafanywa na raia wa taifa hilo. 

Fahamu Ubunifu wa Majiko ya Solar Yenye Uwezo wa Kupika Chakula cha Wanafunzi Zaidi 600 Katika Shule Moja Nchini Tanzania

Na Emmanuel Chibasa 👉Ni teknolojia Yenye Kuleta Suluhisho ya Kupunguza Matumizi ya Kuni na Mkaa Katika Taasisi za Elimu 👉Inawezesha kupika ugali, Maharage,Makande pamoja na wali Kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wengi na wafanyakazi kwa haraka zaidi pamoja na kupunguza gharama za matumizi. Katika dunia ya leo, nishati ya umeme jua inachukua nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto za mazingira, kijamii na kiuchumi na taasisi za elimu zinapokua sehemu ya matumizi haya faida zake zinaonekana wazi. Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni agenda mahususi ambayo imechukua nafasi kubwa katika Sera, Mipango na Mikakati ya Serikali mbalimbali duniani. Umuhimu wa agenda hii unasukumwa na ongezeko la uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia. Umeme jua ni chanzo cha nishati kisichokua na uchafuzi wa mazingira, kwa kutumia paneli za jua, shule zinaweza kupata umeme kwa gharama nafuu kwa ajili ya ...

Uvccm yasema fomu ni moja tu ya urais 2025 kwa pande zote mbili za muungano

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa na Mlezi wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu  Mohammed Ali Kawaida ameweka bayana msimamo wa Umoja wa Vijana wa CCM ya kuwa ifikapo 2025 UVCCM itasimama na Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa Zanzibar na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania "Tunaona kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali zote mbili, ifikapo 2025 Fomu ya Uraisi ni moja tu kwa Zanzibar ni Dkt Mwinyi na Bara ni Dkt Samia na katika hili hatutakuwa wanafiki tutasimama Imara kuyasema yote yaliyofanywa na Viongozi wetu" Kawaida ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mahafali ya UVCCM Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Suza Tunguu Unguja Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2024. Aidha Kawaida amewahimiza vijana wote nchini kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukisemea kwa wananchi wote ili kiendelee kuaminika kwa wananchi na kuendelea kushika Dola. 8 Umoja wa Vijana wa CCM utafanya kazi usiku na mchana kusema mazuri yote yanayofanywa na Serikali zote mbili za...

Mwenyekiti ccm Musoma akumbusha umuhimu wa kufanya mazoezi

Na Shomari Binda-Musoma Viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya Musoma mjini wamekuwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kushiriki mazoezi ya" jogging" yaliyoandaliwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka. Mazoezi hayo yamefanyika leo septemba 28 yaliyoanzia na kumalizikia kwenye uwanja wa posta ambapo licha ya viongozi hao makundi mbalimbali yameshiriki. Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Benedict Magiri amemshukuru na kumpongeza mkuu huyo wa Wilaya kwa kuanzisha utaratibu huo muhimu kwa afya. Amesema mazoezi yana umuhimu mkubwa katika kufanya mwili kuwa na afya njema na kuweza kutekeleza vyema shughuli za kiuchumi. Magiri amesema ilani ya uchaguzi ya CCM inazungumzi pia ushiriki wa michezo na wao kama viongozi wanamuunga mkono kwa kuhamasisha wanachama na wananchi kushiriki mazoezi na michezo. Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kwa upamde wake amesema anataka Musoma iliyochangamka kwa matukio ya mara kwa mara yakiwemo ya kim...

Rais Samia aahidi serikali kufikisha asilimia hamsini kilimo cha umwagiliaji ifikapo 2030

Na NIRC Songea, Ruvuma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imejipanga kuinua Sekta ya umwagiliaji kwa 50%, ifikapo 2030 “Serikali imewekeza katika sekta ya umwagiliaji, na ifikapo 2030, kilimo cha umwagiliaji kinatarajiwa kufikia asilimia 50 ya kilimo nchini”, amesema Rais Samia Samia amesema hayo wakati akihutubia wananchi katika Viwanja vya Majimaji mkoani Ruvuma, ambapo amezungumza na wananchi kuhusu ziara yake hiyo mkoani humo, na kueleza mafanikio, mipango na maagizo mbalimbali ya serikali Rais Samia amesema alikagua ununuzi wa mahindi katika maghala ya NFRA na kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa maghala 28 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 28,000 za mazao ya nafaka, kisha alitembelea shamba la kahawa la Aviv na kusisitiza umuhimu wa kilimo cha kahawa.  Rais Samia ameongeza kuwa Serikali imetoa ruzuku ya mbolea yenye thamani ya bilioni 83.5, huku matumizi ya mbolea yakiongezeka kutoka tani 32,139 mwaka 2022 hadi tani 123,049 mwaka 20...