Rais wa mpito wa Burkina faso aimarisha upatikanaji wa huduma za afya maeneo ya vijijini

GEORGE MARATO TV
0

Rais wa mpito wa Burkina faso kapteni  Ibrahim Traoré amekabidhi magari kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwenye vijiji visivyokuwa na Hospitali.

Magari hayo ambayo ni Hospitali zinazotembea yamekabidhiwa kwa wizara ya afya yakiwa na vifaa tiba vya kisasa pamoja na vitanda vya wagonjwa, Fridge za dawa, Mitungi ya gesi na Jenereta za Umeme. 

Kapteni Traoré ambaye ameliongoza Taifa la Burkina faso tangu septemba 30 mwaka 2022 amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya,elimu pamoja na usalama wa raia na Mali zao.

Kiongozi huyo pia tayari amezifutia leseni za uchimbaji wa madini makampuni yote ya kigeni. 

Amechukua hatua hiyo baada ya kubaini Taifa hilo halinufaiki na madini yanayochimbwa na makampuni ya kigeni ambapo kwa sasa shughuli za uchimbaji madini nchini humo zinafanywa na raia wa taifa hilo. 




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top