Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WANAFUNZI SITA WAFA MAJI WAKIOGELEA BWAWANI

  Watoto sita ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Ochuna Wilayani Rorya mkoani Mara,wafariki dunia kwa kuzama maji wakati wakiogelea. Kwa mujibu wa uongozi wa kata ya Nyaburongo wilayani humo,umesema tukio hilo limetokea leo tarehe 24.08.2024 majira ya saa kumi jioni katika eneo la bwawa la kijiji cha Ochuna. Imeelewa kuwa kuwa wanafunzi wote sita wamefariki bwawani wakitoka majumbani kwao wakaenda bwawani kwa ajili ya kufua nguo kisha walianza kuogolewa katika bwawa hilo lenye tope.  Hata hivyo imeelewa kuwa polisi wamefika baada ya tukio kutokea na miili ya marehemu kwa ajili kuwapeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi (postmortem) Mkuu wa wilaya ya Bw Juma Chikoka,ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama wilaya amethibisha kutokea kwa tukio hilo katika kijiji cha Ochuna na kwamba alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea Amesema baada ya kutukio hilo kutokea wananchi walifika na kuanza kutoa msaada wa kutoa miili hiyo na kwamba serikali imetoa maelek...

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MSIBA WA MKE WA MNADHIMU MKUU WA JWTZ

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 24, 2024 amehani msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi. Akizungumza kwa Niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo.  “Rais Dkt. Samia anatoa rai kwa waombolezaji wote kuendelea kuiombea familia hii katika kipindi hiki cha huzuni”.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara Wajengewa Uwezo na CDF

Na Helena Magabe, Tarime. Waandishi wametakiwa kuandika habari za kuhamasisha Vijana kupima Afya zao na kujikinga na maambukizi ya Ukimwi (VVU) pamoja na kujiepusha na ndoa za utotoni. Wito huo umetolewa kwenye mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Blue sky hotel ambayo yameandaliwa na shirika la utu wa mtoto (CDF) kwa ajili ya kuwajengea uwezo  Waandishi wa habari kuandika habari za Afya ya uzazi na Ukimwi.  Afisa miradi wa CDF  Anold  Masawe ambaye ni mratibu wa mradi wa huduma ya bora za Afya ya uzazi Kwa Vijana amesema vijana ni nyenzo muhimu kuhabarishwa na athari za VVU  pamoja na kujiepusha na ndoa na mimba za utotoni. Amesema elimu inatolewa katika vituo vya Afya 10 na Kata 9 katika Halmashauri ya Tarime Vijijini na tayari vijana 40 wamefundishwa elimu ya afya ya uzazi na VVU ambapo wanatakiwa kuwafikia Vijana 1000 kabla ya mradi huu kuisha ambao ni miaka minne na umebakiza mwaka mmoja. Mratibu wa Mama Halmashauri ya  Wilaya Tarime Bea...

JESHI LA POLISI LAANIKA WATEKAJI...

KISHINDO CHA MJUMBE WA KAMATI KUU CHANG'OA 24 RUANGWA

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ameshuhudia wanachama 24 wa vyama vya CUF na ACT-Wazalendo wakirejea CCM ndani ya siku mbili. Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia wanachama hao wakikabidhi kadi zao kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Abbas Mkwenda (Agosti 23 na 24, 2024) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Mtondo (Kata ya Nambilanje) na Namikulo (Kata ya Chunyu), wilayani Ruangwa, Lindi ambako alifanya ziara ya jimboni kwake. Katika kijiji cha Mtondo, wanachama tisa wa CUF walirejesha kadi zao wakiongozwa na Mzee Bakari Abdallah Nanyambo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nambilanje. Wengine ni Abdallah Ally Manjawila, Bakari Ally Nyanga, Bakari Abdallah Nampota, Mwanahawa Abdallah Komaje, Zaituni Omary Mitachi, Mwanahawa Rashid Chomwingo, Somoe Omary Mkupete na Amina Musa Pachela. Katika kijiji cha Namikulo, wanachama watano wa ACT-Wazalendo walikabidhi kadi zao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Kata ya C...

KISHINDO CHA JWTZ MBELE YA RAIS SAMIA

Amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dr Samia Suluhu Hassan,amesema anaridhishwa na utendaji wa jeshi la ulinzi wa wananchi (JWTZ) na kusema Serikali itatumia kila uwezo wake katika kuimarisha jeshi hilo. Rais Samia ametoa kauli hiyo katika viwanja vya mazoezi ya kijeshi Msata mkoani Pwani,wakati akizungumza na maafisa na wapiganaji wa jeshi hilo wakati wa kufunga zoezi la Medani la miaka 60 ya JWTZ.   Huku akionesha furaha yake baada ya kujionea zoezi hilo la utayari ambalo limefanywa na askari wa JWTZ katika viwanja hivyo vya mapambano,Rais Samia amesema jeshi hilo limeonesha kuwa na uwezo mkubwa hata kuwa mwalimu kwa wengine. Amesema Serikali itaunga mkono juhudi hizo kubwa za ulinzi wa mipaka yete zinazofanywa na JWTZ kwa kuendelea kuliwezesha kwa kukarabati miundo mbinu na kununua zana za kisasa zinazoenda na wakati ili kurahisha utendaji wa kazi. Rais Samia amesema hivi sasa mipaka ya nchi yetu ipo salama na kwamba wakati huu...