WANAFUNZI SITA WAFA MAJI WAKIOGELEA BWAWANI

GEORGE MARATO TV
0

 

Watoto sita ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Ochuna Wilayani Rorya mkoani Mara,wafariki dunia kwa kuzama maji wakati wakiogelea.


Kwa mujibu wa uongozi wa kata ya Nyaburongo wilayani humo,umesema tukio hilo limetokea leo tarehe 24.08.2024 majira ya saa kumi jioni katika eneo la bwawa la kijiji cha Ochuna.


Imeelewa kuwa kuwa wanafunzi wote sita wamefariki bwawani wakitoka majumbani kwao wakaenda bwawani kwa ajili ya kufua nguo kisha walianza kuogolewa katika bwawa hilo lenye tope.


 Hata hivyo imeelewa kuwa polisi wamefika baada ya tukio kutokea na miili ya marehemu kwa ajili kuwapeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi (postmortem)


Mkuu wa wilaya ya Bw Juma Chikoka,ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama wilaya amethibisha kutokea kwa tukio hilo katika kijiji cha Ochuna na kwamba alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea


Amesema baada ya kutukio hilo kutokea wananchi walifika na kuanza kutoa msaada wa kutoa miili hiyo na kwamba serikali imetoa maelekezo ya kuhakikisha jambo hilo halitajirudia.


Walifariki wametajwa kuwa .Eliza jakton okumbe wa darasa la 4,Pendo Emmanuel Nyasanda wa darasa la 4,Anjerina joseph suke wa darasa la 5 ,Yunis jacton okumbe wa darasa la 3.Suzana chacha mwita wa darasa la 3 na Evaline Emmanuel sylvanus wa darasa la 6.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top