KISHINDO CHA JWTZ MBELE YA RAIS SAMIA

GEORGE MARATO TV
0



Amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dr Samia Suluhu Hassan,amesema anaridhishwa na utendaji wa jeshi la ulinzi wa wananchi (JWTZ) na kusema Serikali itatumia kila uwezo wake katika kuimarisha jeshi hilo.

Rais Samia ametoa kauli hiyo katika viwanja vya mazoezi ya kijeshi Msata mkoani Pwani,wakati akizungumza na maafisa na wapiganaji wa jeshi hilo wakati wa kufunga zoezi la Medani la miaka 60 ya JWTZ. 



 Huku akionesha furaha yake baada ya kujionea zoezi hilo la utayari ambalo limefanywa na askari wa JWTZ katika viwanja hivyo vya mapambano,Rais Samia amesema jeshi hilo limeonesha kuwa na uwezo mkubwa hata kuwa mwalimu kwa wengine.


Amesema Serikali itaunga mkono juhudi hizo kubwa za ulinzi wa mipaka yete zinazofanywa na JWTZ kwa kuendelea kuliwezesha kwa kukarabati miundo mbinu na kununua zana za kisasa zinazoenda na wakati ili kurahisha utendaji wa kazi.

Rais Samia amesema hivi sasa mipaka ya nchi yetu ipo salama na kwamba wakati huu ndio wakati sahihi wa kuendelea kuimarisha jeshi hilo.


Amenukuu baadhi maneno ya Baba wa Taifa hayati Mwl Nyerere kuwa wakati wa amani ndio wakati sahihi wa kuliweka jeshi kwenye ari ya utayari.

Kwa sababu hiyo amempongeza mkuu wa majeshi nchini jenerali Jacob John Mkunda kwa uongozi imara katika jeshi hilo huku akiwapongeza askari wanawake ambao wamekuwa hawasiti kuwa mstari wa mbele kwani wanapaswa wajione wao ni askari kama wengine.


Kwa upande wake mkuu wa majeshi jenerali Jacob John Mkunda, pamoja na kumshukuru Rais Samia kwa jinsi anavyoendelea kutoa fedha za kuimarisha jeshi hilo,amesema zoezi hilo ambalo limegharimiwa na Serikali litakuwa kipimo cha jeshi hilo katika medani za kivita.

Amesema jeshi limeendelea kusimamia misingi yake ya kuundwa kwake na kwamba kamwe haliwezi kuwalinda askari wanaokwenda kinyume na misingi hiyo.


Anesema zoezi hilo la medani limefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na JWTZ katika kuelekea kilele chake cha kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake.

Hafla hiyo mbali na kuhudhuriwa na maafisa jenerali,maafisa na askari pia imehudhuriwa na baadhi wakuu wa majeshi na majenerali wastaafu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top