Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SMZ Yavuka Lengo La ilani Ya CCM Katika Viwanda

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imevuka malengo ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 , ambapo ilani ilisema kupima maeneo ya viwanda na kuyaweka tayari  Serikali imetekeleza kwa kupima maeneo hayo, kutayarisha miundombinu ikiwemo ya barabara na miradi ya ujenzi wa  viwanda tayari imeshainiwa.  Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa eneo maalum liliotengwa na Serikali kwa ajili ya viwanda, Dunga Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 7 Agosti 2024. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema  tayari viwanda viwili  vya dawa vimeshatiwa saini leo na  vingine vya magari vinakuja katika maeneo ya Dunga. Vilevile ameeleza kuwa akimaliza awamu ya uongozi mwaka 2025, Serikali itakuwa imeacha alama kwa kukamilisha ujenzi wa viwanda Unguja na Pemba. Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa viwanda yanawekewa miundombinu muhimu iki...

Takukuru Kagera Yaokoa Shilingi Milioni 4.3 Za Tasaf

  Na Angela Sebastian TAASISI ya kupamba na kuzuia Rushwa mkoani  Kagera  (TAKUKURU) imeokoa kaisia cha shilingi milioni 4.3 baada ya kupokea taarifa ya ubadhirifu wa fedha za mfuko wa maendeleo wa kunusuru  kaya maskini (TASAF) kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kumutana kata ya Kibimba Wilayani Ngara mkoani hapa. Ezekia Sinkala naibu mkuu wa taasisi hiyo mkoa wa Kagera alieleza hayo  leo  wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake mjini Bukoba wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu. “Baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kuwa mnamo Septemba 20 mwaka 2020 kulikuwa na zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF katika kijiji  Kumutana ambazo zilikuwa za mwezi Mei hadi Juni na mwezi Julai hadi Agosti ambapo ulikuwa mgao wa madilisha mawili kwa wanufaika 139" Amesema baada ya kufuatilia mwenendo wa ugawaji wa fedha hizo  walibaini fedha zilizokuwa zimechukuliwa na kupelekwa kijijini hapo ziliku...

Balozi Kombo Apokea Hati za Utambulisho Toka Kwa Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zimbabwe nchini, Mhe. Helen Bawange Ndingani, Balozi Mteule wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 5 Agosti, 2024. Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amewapongeza mabalozi hao kwa uteuzi waliuopata na pia amewaahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi watakachokuwa nchini kuziwakilisha nchi zao. Aidha, ameeleza Mabalozi hao Wateule wanatarajiwa kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 na 13 Agosti, 2024.

TFF Yakabidhi JWTZ Mipira 500 Kuendeleza Michezo Kwa Vijana

Shirikisho la soka Tanzania limekabidhi mipira mia tano kwa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania  JWTZ,  kwa ajili ya kuendeleza michezo kwa vijana wenye umri kati ya miaka sita hadi kumi na nne, kupitia vituo maalumu vya mafunzo ya michezo vinavyo tarajia kuanzishwa  na JWTZ. Akikabidhi  sehemu ya mipira mia tano kwa mkuu wa majeshi ya  ulinzi ya wananchi wa Tanzania, Rais wa TFF Wallace Karia, amesema TFF imetoa mipira hiyo katika kutekeleza ahadi yake ya kulisaidia jeshi katika sekta ya michezo hasa wa mpira wa miguu. Karia  ambaye ameambatana na maafisa mbalimbali wa TFF, pamoja na kulipongeza Jeshi la ulinzi la  wananchi wa Tanzania katika kuendeleza mpira wa miguu nchini, amemuomba mkuu huyo  wa Majeshi kufikiria kuanzisha timu za mpira wa miguu za ufukweni (beach soka) ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa. Hata hivyo pamoja na kupongeza jeshi kwa mpango wake wa ujenzi wa vituo hivyo vya mafunzo ya michezo,amesema kuwa huwezi kutaja mpira wa...

Wanachama na Mashabiki wa Timu ya Yanga Igunga Waadhimisha Wiki ya Mwananchi Kwa Kutoa Msaada

Na Lubango Mleka, Igunga. WANACHAMA na Mashabiki wa Timu ya Yanga Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wameadhimisha wiki ya Mwananchi kwa kutembelea wodi ya Watoto katika Hospitali ya wilaya ya Igunga na Gereza la Wilaya ya Igunga na kutoa mahitaji mbalimbali. Kilele hicho kimeanza kwa maandamano ya amani kutokea uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine uliopo Mamlaka ya mji mdogo wa Igunga na kuelekea katika Hospitali ya wilaya ya Igunga na kuwafariji Wazazi na Watoto ambao ni wagonjwa kwa kuwapatia juisi, maji ya kunywa, sabuni za unga na vipande, dawa za miswaki, mafuta pamoja na pampasi.  Wamehitimisha maadhimisho hayo kwa kutembelea Gereza kuu wilaya ya Igunga ambapo wametoa kiasi cha sh. 30,000 kwa ajili ya kununua kifurushi cha Azam ili Wafungwa na Mahabusu wapete fursa ya kufuatilia kilele cha wiki ya Mwananchi, aidha wametoa sabuni za unga na vipande, viwembe, maji ya kunywa na mipira miwili kwa ajili ya kufanya mazoezi.  Mkaguzi Msaidi I. R. Ntandu kwa niaba ya Mkuu wa gereza la w...

Kampeni ya Msaada wa Kesheria ya Mama Samia Inapatikana Kwenye Maonesho ya Nane Nane

Na Mwandishi Wetu BAADA ya kusaidia maelefu ya Watanzania kupitia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia au maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign, sasa iko katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma. Kampeni hiyo ambayo tangu kuzinduliwa kwake mwaka jana, imekuwa ikitumia wabobezi katika tasnia hiyo ya sheria kutatua migogoro mbalimbali inayotokea kwenye jamii katika mikoa mbalimbali wanakopita iko katika maonesho hayo kutoa msaada huo wa kisheria kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo ya nanenane. Mbali na kurejesha tabasamu kwa wananchi wenye migogoro mbalimbali, pia kampeni hiyo imefanyika kama darasa la kutoa elimu kuhusu masuala ya sheria na namna haki inavyoweza kupatikana kwa kutumia sheria hizo. Kampeni hiyo ya Mama Samia Legal Aid Campaign katika maonesho hayo, pia inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za ushauri na ufumbuzi wa matatizo mbalimbali ya kisheria wanayokumbana nayo k...