Na Angela Sebastian
TAASISI ya kupamba na kuzuia Rushwa mkoani Kagera (TAKUKURU) imeokoa kaisia cha shilingi milioni 4.3 baada ya kupokea taarifa ya ubadhirifu wa fedha za mfuko wa maendeleo wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kumutana kata ya Kibimba Wilayani Ngara mkoani hapa.
Ezekia Sinkala naibu mkuu wa taasisi hiyo mkoa wa Kagera alieleza hayo leo wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake mjini Bukoba wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.
“Baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kuwa mnamo Septemba 20 mwaka 2020 kulikuwa na zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF katika kijiji Kumutana ambazo zilikuwa za mwezi Mei hadi Juni na mwezi Julai hadi Agosti ambapo ulikuwa mgao wa madilisha mawili kwa wanufaika 139"
Amesema baada ya kufuatilia mwenendo wa ugawaji wa fedha hizo walibaini fedha zilizokuwa zimechukuliwa na kupelekwa kijijini hapo zilikuwa shilling milioni 9.3 hivyo watumishi walitumia uelewa mdogo wa wanufaika wa mpango huo na kuwalipa hawamu moja tu nyingine wakizitumia wao.
Ametaja idadi ya watumishi hao waliohusika na ubadhirifu huo kuwa ni wanne ambao ni wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutoka katika idara ya maendeleo ya jamii wawili,mwenyekiti wa kijijji na mtendaji wa kijiji hicho ambapo hakuwataja majina yao.
Amesema baada kuhojiwa na Takukuru walikiri na kisha kurejesha kiasi hicho cha fedha ambacho kililipwa tena kwa wanufaika wa mpango huo.
Aidha kwa kipindi cha Aprili hadi Juni taasisi hiyo ilipokea malalamiko 132 ambapo kati ya hayo 48 hayahusiani na Rushwa na 84 yalihusu rushwa uchunguzi wamajalada 11 umekamilika. huku majalada 73 uchunguzi wake ukiendelea.

Comments
Post a Comment